October 15, 2016

BENKI YA POSTA TANZANIA (TPB) YAKABIDHI MRADI WA VYOO SHULE YA MSINGI IPINDA KYELA

Meneja Mahusiano kwa Umma benki ya Posta Tanzania (TPB) Noves Moses akizungumza katika hafla ya Makabidhiano ya mradi wa vyoo vya walimu vyenye matundu matano katika shule ya Msingi Ipinda Wilayani Kyela Mkoani Mbeya ambavyo ujenzi wake umeghalimu kiasi cha shilingi milioni 8kwa msaada wa benki hiyo ya Posta Tanzania.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ipinda Wilayani kyela Mkoani Mbeya wakitoa burudani katika hafla ya makabidhiano ya vyoo vya walimu vyenye matundu matano ambavyo vimejengwa kwa msaada wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa thamani ya shilingi milioni 8.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ipinda Subira Gwakabale akishukuru kwa kupatiwa msaada na benki ya Posta Tanzania (TPB).

Meneja wa benki ya Posta Tanzania (TPB)Mkoa wa Mbeya kulia ,Humphrey Julias akiteta jambo na Meneja Mahusiano kwa Umma wa benki hiyo Noves Moses kabla ya kukabidhi rasmi mradi wa vyoo vya walimu vyenye matundu matano vilivyojengwa katika shule ya Msingi Ipinda Wilayani Kyela Mkoani Mbeya kwa Msaada wa benki hiyo kwa thamani ya shilingi milioni 8.

Meneja Mahusiano kwa Umma wa benki ya Posta Tanzania TPB,Noves Moses akizindua na kukabidhi rasmi mradi wa vyoo vya walimu vyenye matundu Matano ujenzi ambao umeghalimu kiasi cha shilingi milioni8 katika shule ya Msingi Ipinda Wilayani kyela Mkoani Mbeya Otobar 13 mwaka huu,kushoto ni mwenyekiti wa kijiji cha Ipinda Saadat Sam (katikati)Afisa elimu taaluma Lucasian Kavishe na mwalimu Mkuu wa shule hiyo Subira Gwakabale kulia .

Muonekano wa jengo la vyoo vya walimu katika shule ya Msingi Ipinda lenye matundu matano ambalo ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi milioni8.

Meza kuu katika Picha ya pamoja na walimu na wajumbe wa bodi ya shule ya Msingi Pinda.

Meza kuu na wafanyakazi wa benki ya Posta Tanzania TPB tawi la Kyela na Mbeya.

Meza kuu katika picha ya pamoja na wadau na viongozi wa serikali ya kijiji cha Ipinda Wilaya ya Kyela.

Vyoo vilivyokuwa vikitumiwa na walimu wa shule ya Msingi Ipinda kabla ya kujengewa vyoo vipya na benki ya Posta Tanzania (TPB). Picha na E.Madafa.

No comments:

Post a Comment

Pages