October 16, 2016

GLOBAL PEACE FOUNDATION TANZANIA WATOA ELIMU JUU YA KUDUMISHA AMANI KATIKA FAMILIA , JUKWAA LA VIJANA JIJINI DAR

Kila Baada ya Mwezi kikundi cha Tandale Youth Development Centre hufanya Jukwaa la Vijana ambapo vijana hukutana na kujadili mambo mbalimbali yanayohusiana na wao. Katika jukwaa la mwezi huu kulikuwa na mada inayosema: "Nafasi  ya mtoto wa kike katika jamii" ambapo majadiliano yalilenga zaidi kutambua nafasi hizo, changamoto wanazokutana nazo watoto wa kike pamoja, namna ya kuzitatua na jinsi gani mtoto wa kike anavyoweza kusimamia malengo yake kufanikiwa.

Aidha katika jukwaa hilo la vijana Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation  kupitia Mkurugenzi Mkazi wa hapa nchini, Martha Nghambi alitoa pia elimu ya nafasi ya mzazi katika kudumisha  amani ndani ya familia, ambapo alisema kuwa ili amani iweze kudumishwa na watu waishi bila kuwepo na mifarakano ni lazima kujenga mahusiano mazuri kuanzia chini yaani wanafamilia kuweza kuelewena kwa kuwahusisha wazazi na watoto ambapo hawa wakiishi vema basi hakutakuwa tena na uvunjifu wa amani na kusisitiza kuwa kila mtu analojukumu la kulinda amani.
Mwendeshaji wa Jukwaa la Vijana lililofanyika Tandale leo Jamal Magabilo akitoa neno la utangulizi na kuwakaribisha wageni waalikwa wote katika jukwaa
Mkurugenzi wa Gida Rahma Bendera akiitambulisha rasmi mada katika Jukwaa la vijana inayosema nafasi ya mtoto wa kike katika jamii
Mkurugenzi Mkazi wa Global Peace Foundation Tanzania Bi. Martha Nghambi akitoa Elimu kwa kina juu ya nafasi ya mzazi katika kudumisha amani kwenye familia ambapo aligusia mambo mengi ikiwa ni pamoja na visababishi vya uvunjishi wa amani pamoja na namna ya kuzuia uvunjifu huo wa amani katika familia.
Mwandaaji wa Matukio wa TYDC Imani akitoa neno la shukurani kwa wote waliohudhulia jukwaa hilo
Afisa Mahusiano wa TYDC Anna Emmanuel akielezea historia fupi ya umoja wao
Mdahalo ukiwa umeanza
Loveness Msuya akizungumzia mada inayohusu jinsi gani mtoto wa kike anaweza kusimama kwenye ndoto na malengo yake na mwisho wasiku kufanikiwa, alieleza njia na mbinu mbalimbali zinazoweza kumfikisha mtoto wa kike kule anapo pataka.
Anna Mwalongo kutoka DUCE akisisitiza kwa nguvu na kupaza sauti ya kuwasihi Mabinti kujitambua ili waweze kuepukana na vishawishi mbalimbali vinavyo sababishwa na vijana.
 Ni Binti Mdogo mwenye umri wa miaka 12 na mwenye upeo mkubwa Zurpha Issa yeye alitaka kujua ni namna gani anaweza vipi kujizuia na mabadiriko yake? ambapo pia alieleza kuwa yeye anandoto ya kuwa msanii hapo baadae.
Mkurugenzi Mkazi wa Global Peace Foundation Tanzania Bi. Martha Nghambi  akifuatilia kwa makini mdahalo huo
Steven Mfuko Maarufu kwa Jina la Babu Zero akichangia mada katika mdahalo huo ambapo alizungumzia changamoto za mabinti kuvunja ungo wakiwa katika umri mdogo na kuelezea namna vijana wanavyo warubuni na kuwadanganya mabinti wadogo.
Bi Stella Francis Mganga akielezea jinsi mabadiliko makubwa ya Teknolojia yalivyo na yanavyo endelea kuporomosha maadili ya vijana wengi na kutumia muda wao mwingi huko kulipo kufanya maswala mengine.
Mhandisi Eliwanjeria James  kutoka Kikundi cha Mainjinia wanawake Tanzania  akichangia mada katika jukwaa hilo.
Asha Furaha mkazi wa Tandale akieleza mambo mbalimbali yanayowakabili mabinti na kuwasihi kuendelea kupata elimu zaidi juu ya usichana wao.
Vijana, Wazazi na wadau mbalimbali wakiwa katika jukwaa hilo.
 Picha ya Pamoja.
Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa

No comments:

Post a Comment

Pages