October 10, 2016

KAMPUNI YA CRCC KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU MKOANI DODOMA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Ujenzi ya CRCC ya China Bw. Fengchao Meng ambaye ameahidi kuwekeza kwa kushirikiana na Serikali katika kuboresha miundombinu ya mkoa wa Dodoma.

Mwenyekiti huo ambaye aliongozana na Mwenyekiti wa Kampuni nyingine ya Ujenzi ya CCECC ya China, Bw. Yuan Li pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha  Urafiki kati ya Serikali za Tanzania na ChinaBw. Joseph Kahama .

Akizungumza na Bw. Meng leo (Jumatatu, Oktoba 10, 2016) ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu amesema kipaumbele cha Serikali kwa sasa ni uendelezaji wa Makao Makuu Dodoma.

Aliongeza kuwa China na Tanzania ni marafiki wa muda mrefu na mataifa hayo yanashirikiana vizuri katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali hivyo Serikali inatarajia mengi kutoka kwenye kampuni hiyo kupitia kwa mwenyekiti wake Bw. Meng.

“Dodoma kuna fursa za uwekezaji kwenye sekta nyingi kama miundombinu, kilimo na viwanda.Mnaweza kuwekeza kwenye ujenzi wa nyumba za makazi, ofisi, huduma za kijamii na viwanda ,”

Kwa upande wake Bw. Meng amesema kampuni yake itaungana na Serikali katika kuboresha Makao  Makuu ya Serikali na inatarajia kutuma wataalam wake mkoani Dodoma kuangalia maeneo ya uwekezaji.

‘Nataraji tutakuwekeza katika ujenzi wa miundombinu, nyumba za makazi, ofisi, maeneo ya kutolea huduma za jamii na teknolojia zitakazowezesha upatikanaji wa maji safi na salama.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATATU, OKTOBA 10, 2016.

No comments:

Post a Comment

Pages