OMUTWALE Paschal
Rutaihwa Kakiziba
13
JULAI 1935 – 28 OKTOBA 2004
Baba
yetu mpendwa umetimiza mwaka wa 12 tangu ulipotwaliwa na Bwana. Picha yako
inatukumbusha uwepo wako tulipokuwa sote hapa duniani, na hasa ukarimu, upendo,
upole, uchangamfu na wingi wa busara.
Ni
vigumu kukubali kwamba haupo nasi lakini hatuna budi kuamini kwamba uko nasi
kiroho kwa vile tunaye Mungu ambaye anaendelea kututia nguvu kila iitwapo leo.
Busara zako na ucheshi wako vinazidi kutuimarisha kila siku na tunaendelea
kuzingatia maneno yako uliyokuwa ukihimiza juu ya kuwa na upendo na umoja
katika familia huku tukiendelea kumtumaini Mungu wetu ambaye amekuita kwake.
Mke
wako Mary-Hilda Kakiziba, rafiki yako Galita, watoto wako, wajukuu, wakwe zako,
dada zako, kaka zako na wadogo zako, ndugu, marafiki na majirani wanakosa
ucheshi na ushauri wako na wanakukumbuka daima.
MISA YA KUMBUKUMBU
ITAFANYIKA JUMAPILI, OKTOBA 30, 2016, SAA 3 ASUBUHI KWENYE KIGANGO CHA MT.
ANTHONY WA PADUA, BOKO, DSM.
Tumaini letu linajengwa na neno lisemalo: ”Umevipiga vita vilivyo vizuri,
mwendo umeumaliza na imani umeilinda” (2Tim. 4:7)
Tunakuomba Ee Bwana uendelee kuipumzisha roho yake
mahali pema peponi, AMEN.
No comments:
Post a Comment