October 30, 2016

MUSWADA WA HUDUMA WA HABARI WA MWAKA 2016

Na Mwandishi Wetu

Akiongea wakati wa kipindi cha jicho letu la habari kinachorushwa na star tv Mwandishi Mwandamizi Bw.Pascal Mayala amesema kuwa waandishi wa habari wamekuwa wakiupinga muswada huu bila kuangalia faida zilizopo ndani yake ikiwamo uboreshwaji wa maslahi na mafunzo kwa waandishi wa habari.


"Waandishi wa habari wamekuwa wakikaa na kuukosoa muswada huu bila kuangalia nini kipo ndani, kiukweli muswada huu unatotauti Sana na Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 tunaoutumia sasa, unafaida nyingi kwa waandishi na utawasaidia kukua kiuandishi". Alisema Bw. Mayala.


Bw.Mayala aliongeza kuwa muswada huu utawezesha kuwapata waandishi walioelimika kutokana na uwepo wa vifungu vinavyowawezesha waandishi kupata mafunzo katika maeneo yatakayowawezesha kukua kitaaluma.

Naye Mwandishi Mwandamizi Bw.Derek Murusuri amesema kuwa Sekta ya habari nchini imekuwa na changamoto zakiutendaji kwa muda mrefu jambo ambalo linakuja kutatuliwa na muswada wa huduma za habari ya mwaka 2016.

Bw.Derek alisema kuwa muswada huu kwa kiasi kikubwa umejikita kutatua chamgamoto zilizokuwa zikiwakabili waandishi ikiwemo masuala ya mikataba na bima kwa waandishi wa habari.

"Tumeshudia tasnia yenye changamoto nyingi kwa waandishi wa habari kwa kipindi cha muda mrefu na malalamiko yamekuwa ni mengi hasa kwenye masuala yanayohusu maslahi ya waandishi wa habari"-Alisema Bw.Derek.

Mwandishi wa habari Juma mudimi amewataka waandishi wa habari kuusoma muswada huo na kuacha kupotosha watu juu ya vifungu vilivyopo ndani ya muswada huo.

Akizungumzia kuhusu Kuongezwa kwa muda Edwin Soko amesema suala hilo lisiwe ajenda bali kuusoma na kuuelewa kwa maslahi ya tasnia.

No comments:

Post a Comment

Pages