Nahodha wa timu ya gofu ya NMB, George Kivaria akipiga mpira wakati wa michuano ya NMB Monthly Mug iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya gofu Lugalo jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na Benki ya NMB. (Na Mpiga Picha Wetu)
NA SALUM MKANDEMBA
NA SALUM MKANDEMBA
MASHINDANO ya mchezo wa gofu ya NMB Monthly Mug, yamefanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Gofu Lugalo, ambako jumla ya wachezaji 60 walichuana.
Mashindano hayo yanayodhaminiwa na Benki ya NMB, hufanyika kila mwisho wa mwezi uwanjani hapo, yakishirikisha wachezaji nyota wa timu za NMB na Jeshi Lugalo.
Akizungumza wakati wa michuano hiyo, Nahodha wa Klabu ya Gofu ya NMB, George Kivaria, alisema michuano hiyo imekuwa ikifana kila mwezi, huku ubora na ushindani ukiimarika.
Kivaria alisema ya kuwa, michuano hiyo uhusisha timu za wakubwa na wadogo, ambako asubuhi huwa zamu ya wakubwa, wakati mchana hadi jioni huwa zamu ya vijana wadogo.
Aliwataka wachezaji wa mchezo huo kujitokeza kwa wingi kushiriki NMB Monthly Mug, kwani yamekuwa jukwaa huru la nyota wa gofu kuboresha viwango vyao vya mchezo huo.
Aliwatoa shaka Watanzania wanaouogopa mchezo huo wakidhani ni wa kitajiri, kwa kuwaambia NMB imefuta tabaka hilo na kuugeuza kuwa mchezo unaoweza kuchezwa na jamii zote.
“Udhamini wa NMB katika mashindano haya, umebadili taswira ya gofu. Sasa unachezeka hata na watu wa kada ya chini, ambao awali walikuwa wakiuogopa mchezo huu,” alisema Kivaria.
Michael Misabo ambaye ni mchezaji wa kikosi cha NMB, alibainisha kuwa ushindani uliopo katika michuano hiyo ni mkubwa, huku akiwataka nyota mbalimbali wa gofu kujiuunga nao.
“Hapa kuna timu mbili za Jeshi Lugalo na NMB. Hii ya Jeshi Lugalo inahusisha maofisa wa jeshi na wanajeshi, lakini hii ya NMB inahusisha wachezaji wa kiraia.
“Hivyo wachezaji wa kiraia wajitokeze kuungana nasi katika michuano hii ya kila mwisho wa mwezi, ambayo kupitia udhamini wa NMB, imeifanya kwa ya ushindani,” alisema Misabo.
No comments:
Post a Comment