October 19, 2016

TANESCO YAKAMATA VIFAA VYA UMEME YENYE THAMANI YA TSH 61,000,000

 Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Leila Muhaji akizungumza na waandishi wa kuhusu wizi huo wa vifaa vya umeme vyenye thamani ya milioni 61 na kukamatwa, Kulia ni Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Lucas Mkondya.
  Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Lucas Mkondya.(wa pili kushoto) akiwa na waandishi na walinzi wa Tanesco.
  Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Lucas Mkondya.(wa pili kushoto) akiwa na waandishi.
  Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Lucas Mkondya.(wa pili kushoto) akiwa na waandishi.
 Gari la Tanesco likiwa na shehena ya vifaa vilivyoibwa  Kikuu cha Polisi Dar es Salaam.
Gari la Tanesco likiwa na shehena ya vifaa vilivyoibwa  Kikuu cha Polisi Dar es Salaam. 

Mwandishi Wetu.

Tarehe 18-10.2016 saa 10;00 jioni maeneo ya Salasala Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Polisi wakishirikiana na Kikosi kazi cha kuzuia uharibifu wa miondo mbinu ya Shirika la umeme Tanzania Tanesco lilipata taarifa toka kwa raia mwema kuwa kuna watu wanaohujumu miundo mbinu ya Shirika hilo.

Kikosi hicho kilifika eneo hilo katika nyumba ya Willfred Barutti (45) mkazi wa Makumbusho na kufanya upekuzi kwenye nyumba hiyo ambapo walivipata vifaa mbalimbali Line Meterial ambavyo hutumika kwa ajili ya kuunganisha umeme vya Kampuni ya Tanesco.Polisi walikwenda katika nyumba nyingine mali ya Betrice Emmanuel (42) mkazi wa Salasala Mabanda wakafanya upekuzi na kufanikiwa kukamata vifaa vifuatavyo;

Nyaya aina ya Drums'02,roller ya waya aina ya AICC ya umeme wa 50 mm ambazo hutumiwa na tanesco kituo cha Kilimahewa huko Kawe Wilaya ya Kinondoni.

Thamani ya vifaa hivyo vinakadiliwa kuwa Tsh.61,000,000,Watuhumiwa wawili wanashikiliwa kwa mahojiano na Upelelezi utakapokamilika watapelekwa mahakamani kwa hatua za kisheria.

No comments:

Post a Comment

Pages