October 22, 2016

UZINDUZI WA TAARIFA YA HALI YA IDADI YA WATU DUNIANI

 Wananchi wa kijiji cha Kilombero, Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja wakifuatilia kwa makini yaliyokua yakijiri wakati hafla ya uzinduzi wa taarifa hiyo.  
 Mhe. Salama Abuu Talib, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Zanzibar akihutubia wananchi waliohudhuria sherehe hizo.
 Mhe. Issa Juma Ally, Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B, akitoa neno kwa wananchi waliohudhuria uzinduzi wa Taarifa hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ili aweze kuongea na wananchi na kuizindua rasmi.
 Mgeni Rasmi Mhe. Thabit Kombo, Waziri wa Afya, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akieleza juu ya fursa ndogo waliyonayo wasichana ya kumaliza skuli kuliko wavulana na wako katika hatari zaidi ya kukabiliwa na ndoa za utotoni, ajira za watoto, ukeketaji na matendo mengine ya udhalilishaji.
 Mhe. Thabit Kombo, Waziri wa Afya, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Taarifa ya Hali ya Idadi ya Watu Duniani.
Mgeni Rasmi Mhe. Thabit Kombo, Waziri wa Afya, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akiwaonyesha wananchi kitabu cha Taarifa ya Hali ya Idadi ya Watu Duniani mara baada ya kuizindua. 

No comments:

Post a Comment

Pages