Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe
anatarajia kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa
Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU)
itakayofanyika Oktoba 21 mwaka huu katika Ukumbi wa Karimjee.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam Makamu
Mwenyekiti wa Tume wa Haki za Binadamu na Tawala Bora,Idd Mapuri
alisema maadhimisho hayo yatakayayo
washirikisha viongozi ,wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali ndani na nje ya
nchi.
Alisema
kongamano hilo litakalojadili mada
mbalimbali kuhusu utawala bora na utawala wa sheria nchini.
“Miongoni
mwa mada zitakazowasilishwa ni pamoja na chimbuko,changamoto na mafanikio ya TKU iatakayotolewa na Jaji Mstaafu wa
Mahaka Kuu Gad Mjemmas , mada nyingine ni
uzoefu wa Afrik wa Taasisi za ‘Ombudsman’ itakayotolewa na muwakilishi kutoka Jumuiya
ya Taasisi za Uchunguzi na Profesa Paramagamba Kabudi wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM) atawasilisha mada ya kutoka kwaTKU changamoto zilizopo na
matarajio,”alisema Mapuri.
Aidha
alisema Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Damianu Lubuva
atatoa hotuba itakayoeleza uzoefu wake TKU.
Alisema
kauli mbiu ni “Utawala wa Sheria ndiyo msingi Mkuu wa utawala bora”.
No comments:
Post a Comment