November 22, 2016

MAJALIWA AMJULIA HALI BABA MZAZI WA WAZIRI MKUU MSTAAFU MIZENGO PINDA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia jambo kati yake na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda baada ya kuwasili kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma ambako alikwenda kumjulia hali baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee Xavery Kayanza Pinda Novemba 22, 2016. Kulia ni Paroko wa Kanisa Kuu Katoliki la Dodoma , Padri Wisi Onesmo na wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakati alipokwenda kwenye hospitali ya Mkoa wa Dodoma kumjulia hali baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee Xavery Kayanza Pinda Novemba 22, 2016.
 Waziri Mkuu, Kaasim Majaliwa  akiongozana na  Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kuelekea wodini wakati alipokwenda kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma kumjulia hali Mzee Xavery Kayanza Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu Novemba  22, 2016. Mzee Pnda amelazwa kwenye hospitali hiyo kwa matibabu. 
  Waziri Mkuu, Kaasim Majaliwa  akiteta  na  Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda  wakati alipokwenda kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma kumjulia hali Mzee Xavery Kayanza Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu Novemba  22, 2016. Mzee Pinda amelazwa kwenye hospitali hiyo kwa matibabu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

Pages