November 04, 2016

WANANCHI KIJIJI CHA MKALAMA WAUNGA MKONO KAMPENI ZA MKUU WA WILAYA YA HAI ZA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA

Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mkalama waliojitokeza kuunga mkono kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa iliyozinduliwa hivi karibuni wilayani humo.
Afisa tawala wa wilaya ya Hai,Julieth Mushi akishiriki katika zoezi la ubebaji wa mawe kwa ajili ya ujenzi wa msingi katika shule hiyo.
Katibu tawala wa wilaya ya Hai,Upendo Wela akishiriki katika usombaji wa mawe kwa ajili ya ujenzi wa msingi katika shule mppya ya Kilima Mswaki.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mkalama wilayani Hai wakishiriki kuvunja na kubeba mawe kwa ajili ya ujenzi wa msingi wa madarasa katika shule mya ya Kilima Mswaki iliopo kijijini hapo.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akiwa amebeba jiwe kubwa ikiwa ni kuonesha kwa vitendo namna viongozi wa serikali wameamua kushirikiana kwa vitendo na wananchi katika kujiletea maendeleo.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akishiriki katika kuchimba msingi katika shule mpya ya Kilima Mswaki wakati wa kuanza kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Katibu tawala wa wilaya ya Hai Upendo Wela akishiriki kuchimba msingi katika shule hiyo.
Sehemu ya Msingi ulianza kuchimbwa katika shule mpya ya Kilima Mswaki iliyopo katika kijiji cha Mkalama.
Sehemu ya Mawe yaliyokusanywa kwa ajili ya ujenzi wa msingi katika shule ya Kilima Mswaki .
Moja ya Madarasa yaliyojengwa kwa nguvu ya wananchi katika eneo la Kilima Mswaki kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wanaotembea umbali mrefu kufuata shule moja pekee ya Mkalama iliyopo katka kijiji hicho.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akizunumza katika kikao na wanachi wa kijiji cha Mkalama mara baada ya kushiriki zoezi la uchimbaji na ujenzi wa msingi kwa ajili ya madarasa katika shule ya msingi ya Kilima Mswaki.
Baadhi ya wnachi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kuhusu kuchangia katika ujenzi wa madarasa katika kijiji cha Mkalama wilayani Hai.
Katibu tawala wa wilaya ya Hai,Uoendo Wela akizungumza wakati wa kikao hicho.kulia ni mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Bakanwa.
Baaadhi ya Wananchi.
Baadhi ya wananchi wakicahngia fedha katika harambee ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Kilima Mswaki iliyopo katika kijiji cha Mkalama wilayani Hai. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini                          

No comments:

Post a Comment

Pages