January 27, 2017

Benki ya Kilimo yajidhatiti kuwainua wakulima

Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TABD) Bw. Francis Assenga akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es saalam kuhusu mikakati ya Benki hiyo kuwainua wakulima wadogo ili waweze kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda. Kushoto ni Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha wa Benki hiyo, Bw. Albert Ngusaru. 

 Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji  wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TABD) Bw. Francis Assenga akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam ambapo alibainisha kuwa Benki hiyo imekuwa ikitoa mikopo kwa wakulima ili kuziba pengo la upatikanaji wa fedha kwenye minyororo ya thamani katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi na mazao ya misitu. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara Bw. Geofrey Mtawa na kushoto Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha Bw. Albert Ngusaru.
 Kaimu Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara Bw. Geofrey Mtawa akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu mpango wa Benki hiyo kuhakikisha kuwa wakulima wote wanawezeshwa ili kuinua kilimo hapa nchini. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji  wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TABD) Bw. Francis Assenga.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania leo Jijini Dar es salaam. (Picha na Frank Mvungi- Maelezo)

No comments:

Post a Comment

Pages