Klabu ya golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania imetuma salam za rambirambi kwa Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Uhuru,Burudani na Mzalendo kufuatia kifo cha Mwandishi wake wa habari za michezo Amina Athumani.
Akizungumza katika Kikao cha maandalizi ya kuelekea maadhimisho ya Miaka 10 ya klabu hiyo mahiri ya golf nchini Mwenyekiti wake Brigedia Jenerali Michael Luwongo alisema kifo hicho si pigo kwa kampuni yake pekee bali na Klabu ya Lugalo ambayo amekuwa akijitokeza katika mashindano Mbali mbali yaliyoandaliwa na klabu hiyo.
“Niseme ukweli tangu nimekuwa mwenyekiti miongoni mwa Waandishi waliozoeleka kuandika michezo mingine hasa soka walianza kutupia macho na Golf ni pamoja na Amina ambaye alikuwa hakosi katika mashindano ya Golf”,Alisema Brigedia Jenerali Luwongo.
Katika Salamu hizo ambazo pia zimekwenda kwa Mwenyekiti wa wa Chama cha Waandishi wa habari za Michezo (TASWA) Juma Pinto ambapo Brigedia Jenerali Luwongo alisema hakika kifo hicho kimepunguza idadi ya waandishi wa habari wanaoangazia mchezo huo.
Brigedia Jenerali Luwongo aliongeza kuwa ni kipindi kigumu kwa familia ndugu na marafiki hivyo amewataka kuwa na moyo wa subira katika kipindi hichi kigumu kwa wanamichezo.
“Binafsi naweza kusema shujaa aliyefia katika mapambano lakini hatuwezi kupingana na mipango ya mungu nilipokea kwa masikitiko taarifa ya kifo chake tasnia na Uhuru publication imepoteza mwanahabari mahiri”Alisema Brigedia Jenerali Luwongo.
Taarifa zinasema Amina Alifariki Dunia Jumapili January 15,2017 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Mnazi mmoja Zanzinzibar alikokwenda kwa ajili ya kuripoti michuano ya Mapinduzi.
Amina alijifungua mtoto ambaye alifariki muda mfupi baada ya kuzaliwa na mpaka mauti yanamkuta alikuwa mwandishi wa michezo wa kampuni ya Uhuru publications.
Mungu ailaze roho ya marehemu Amina Athumani anayetarajiwa kuzikwa mkoani Tanga mahala pema panapostahili.
No comments:
Post a Comment