January 24, 2017

MAKAMU WA RAIS KUZINDUA KAMPUNI YA UWEKEZAJI YA TCCIA INVESTMENT UANDIKISHWAJI KATIKA SOKO LA MITAJI NA DHAMANA DAR ES SALAAM

Zaidi ya Shilingi bilion 45 zinatarajiwa kukusanywa katika kipindi cha wiki sita, wakati wa Kampuni ya uwekezaji ya Taasisi ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA - INVESTMENT) itakapoingia kwenye uuzaji wa hisa kwenye Soko la Mitaji na Dhamana DSE.

Kiasi hicho cha fedha kinatarajiwa kutumiwa kwenye miradi ya uwekezaji katika mikoa ya Mtwara, Dar es salaam, Tanga na Dodoma ili kuongeza mtaji wa kampuni hiyo inayomilikiwa na wazalendo ikiwa na mtaji wa shilingi bilion 28..

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Januari 25 anatarajiwa kuzindua rasmi uandikishwaji wa hisa kwenye soko la Mitaji na Dhamana la Dar es salaam, wa  Kampuni ya uwekezaji ya Taasisi ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA - INVESTMENT) ili kutoa fursa kwa watanzania wengi zaidi kuwekeza kwenye kampuni hiyo iliyoanzishwa mwaka 2005.


Kupitia uuzaji wa hisa za TCCIA  INVESTMENT kwenye soko la mitaji na dhamana la Dar es salaam, Mtaji utakaopatikana unakusudiwa kuwekezwa kwenye uanzishaji wa viwanda pamoja na uwekezaji wa majengo hatua itakayosaidia kutoa fursa za ajira kwa watanzania wengi zaidi na kukuza uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TCCIA  INVESTMENT,  Aloys Mwamanga akizungumza na waandishi wa jijini Dar es Salaam leo kuhusu uzinduzi rasmi wa uandikishwaji wa hisa kwenye soko la Mitaji na Dhamana la Dar es salaam, wa  Kampuni ya uwekezaji ya Taasisi ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA - INVESTMENT) ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
 Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TCCIA  INVESTMENT, Hanim Babiker akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi huo. 
 Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji TCCIA INVESTMENT, Prof. Lucian Msambichaka akifafanua jambo.  
Mjumbe wa Kamati ya Uwekezaji TCCIA Investment, Arphaxad Masambu akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

No comments:

Post a Comment

Pages