January 24, 2017

NAIBU WAZIRI MASAUNI AKAGUA VIPENYO VYA MPAKA WA KASUMULU UNAOTENGANISHA NCHI YA TANZANIA NA MALAWI

 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipokea salamu za heshima baada ya kuwasili kituo cha Uhamiaji Kasumulu, kinachosimamia masuala ya uingiaji na utokaji nchini kwa wananchi wa Nchi za Tanzania na Malawi. Kulia ni Afisa Uhamiaji Mfawidhi wa kituo hicho, Kamishna Msaidizi Taniel Magwaza. Naibu Waziri yupo wilayani Kyela kwa ziara ya kikazi. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto),  akikagua hati ya kusafiria ya mwananchi kutoka nchi ya Malawi, Miston Chikankheni aliyekuwa anaingia  nchini katika Kituo cha Uhamiaji Kasumulu, wilayani Kyela mkoa wa Mbeya. Naibu Waziri yupo wilayani Kyela kwa ziara ya kikazi. 
 Mrakibu Mwandamizi wa Idara ya Uhamiaji, Gragiza John  akijibu maswali aliyoulizwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto) ,baada ya kutembelea moja ya vipenyo vinavyopitisha wahamiaji haramu kutoka Malawi katika mpaka wa Kasumulu. Naibu Waziri ameiagiza  idara hiyo wakishirikiana na Jeshi la Polisi kudhibiti njia hizo ili kuzuia uingiaji wa wahamiaji hao, wakati wa ziara ya kikazi wilayani Kyela.
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji jijini Mbeya, Kamishna Msaidizi, Asumsio Achachaa, akizungumza na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) baada ya kutembelea mpaka waKasumulu unaotenganisha nchi za  Tanzania na Malawi wilayani Kyela. Mlima unaoonekana nyuma upo nchini Malawi. Naibu Waziri yupo wilayani Kyela kwa ziara ya kikazi. 
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI- WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

Post a Comment

Pages