JESHI la Polisi mkoa wa Iringa linamshikilia mkazi wa Mtwivila kata ya Mkimbizi manispaa ya Iringa, Emmanuel Mkiwa (17) kwa kosa la kumlawiti mdogo wake mwenye umri wa miaka 3.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Julius Mjengi alithibitisha kukamatwa kwa kijana huyo.
Alisema kuwa ni kweli kijana huyo amekamatwa juzi kwa tuhuma za kumlawiti mdogo wake mwenye miaka mitatu (jina limehifadhiwa), hivyo hatua zaidi zinaendelea kuchukuliwa.
“Kwa sasa tunakamilisha mchakato wa kukamilisha upelelezi na muda si mrefu tutampeleka mahakamani,” alisema.
Akieleza tukio hilo, Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alibainisha kuwa hatua ya kukamatwa kwa kijana huyo inatokana na taarifa zilizotolewa na wasamalia wema.
Kasesela alibainisha kuwa juzi majira ya saa mbili usiku katika eneo la Mkimbizi, kijiji cha Mtwivila Jeshi la Polisi na maofisa wa serikali walivamia nyumba ya Mzee Shukuru Mkiwa ambaye ni baba wa mtoto aliyelawitiwa na aliyelawiti.
Alisema kuwa baada ya kufika nyumbani hapo walimkuta Shukuru akiwa na watoto wake watatu, huku aliyefanya kitendo cha kulawiti akitaka kukimbia.
Katika mchakato huo, ambapo Kasesela alimbata na Ofisa wa maendeleo ya Jamii Manispaa, alisema kuwa walifanikiwa kumdhibiti kijana huyo pamoja na baba yake, kisha kuwafikisha Polisi.
“Baada ya kuwadhibiti tulimchukua mtoto huyo na kumpeleka Hospitalini ya Rufaa Iringa, alipopimwa ilibainika amepata michubuko mikali sehemu ya mwili wake ikiwemo ya sehemu za siri, na kubainika kuwa amelawitiwa” alisema.
Baadhi ya majirani waliliambia gazeti hili kuwa, waliwahi kumpa taarifa Shukuru kwamba kijana mkubwa ana mtesa mdogo wake, lakini alikuwa akimchapabila kujua kwamba alikuwa akimlawiti kwa muda mrefu.
Pia baadhi waliliambia gazeti hili kuwa Shukuru aliowa mke aliyemzalia watoto watatu akiwemo mtoto huyo mkubwa aliyemlawiti mdogo wake.
Kutokana na kufiwa na mke wake, Shukuru alioamwanamke mwingine ambaye alimzalia mtoto huyo wa miaka mitatu ambaye ndiye amelawitiwa.
Inadaiwa kuwa Mama wa mtoto alitoroka na kumtelekeza mtoto akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu ambapo alikuwa akila ugali tangu alipokuwa mdogo.
No comments:
Post a Comment