Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango (kulia) akizindua nembo mpya na jina jipya la iliyokuwa Benki ya Posta Tanzania na sasa inajulikana kama TPB Bank Plc, ikiwa ni mabadilko yaliyofanywa
baada ya benki hiyo mwaka jana kuorodheshwa chini ya sheria ya makampuni. Benki hiyo ambayo ina miaka 92 tangu kuanzishwa
kwake, ilibadilishwa uendeshaji wake baada ya mwaka 2015, Bunge kufuta sheria
iliyoanzisha benki hiyo na kuifanya kuwa kampuni ili kusajiliwa chini ya Sheria
ya Makampuni, mchakato uliokamilika mwishoni mwa mwaka jana na kwa sasa inaitwa
TPB Bank Plc.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Bank, Sabasaba Moshingi akizungumza wakati wa uzinduzi wa jina hilo jipya na nembo ya Benki hiyo Dar es Salaam leo.
“Benki iliamua kubadilisha nembo ili kwenda sambamba na jina hilo na mabadiliko ya kuboresha benki ili yanayoendelea,” alisema Moshingi na kuongeza kuwa kwa sasa wako katika mchakato wa kujiorodhesha kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) na kuwa ni fursa ya Watanzania kununua hisa katika benki hiyo ambayo faida yake imekuwa ikikua kila wakati.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, TPB Bank, Profesa Lettice Rutashobya akizungumza.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, akizungumza na kuipongeza TPB Bank kwa hatua iliyofikia na kusema kuwa serikali iko katika mikakati ya kuhakikisha nchi inafikia uchumi wa
viwanda ifikapo mwaka 2025, na kuwa sekta ya fedha ambayo inakuwa kwa kasi ina
mchango mkubwa katika kufikia azma hiyo.
No comments:
Post a Comment