January 26, 2017

UNFPA YATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUTUNZIA KUMBUKUMBU ZA MAKOSA YA UKATILI WA KIJINSIA


Mkurugenzi Mtendaji wa Children's Dignity Forum, Koshuma Mtengeti akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya kutunzia kumbukumbu za makosa ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto kutoka UNFPA. (Picha na Francis Dande).
 Kamishna Msaidizi wa Polisi, Mary Nzuki akizungumza katika hafla hiyo.
Mwakilishi Msaidizi wa UNFPA, Christine Kwayu, akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya kutunzia kumbukumbu za makosa ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto kutoka UNFPA. 
 Naibu Kamishna wa Polisi, Mary Nzuki akipokea kompyuta mpakato.
 Naibu Kamishna wa Polisi, Mary Nzuki akipokea kwa furaha sehemu ya msaada wa vifaa vya kutunzia kumbukumbu za makosa ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto kutoka kwa Mwakilishi Msaidizi wa UNFPA, Christine Kwayu, hafla hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Children's Dignity Forum, Koshuma Mtengeti.

Na Mwandishi Wetu

JESHI la Polisi la Tanzania limesema linatarajia kuanza kutunza kumbukumbu za matukio ya ukatili wa kijinsi dhidi ya watoto na wanawake kwa njia ya kielektoniki.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati akipokea vifaa vya kielektoniki kwaajili ya kutunza kumbukumbu hizo kutoka kampuni ya Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Mkuu wa Dawati la Jinsia Makao Makuu DCP Maria Nzuki alisema mpango huo utasaidia kuwapo na takwimu sahihi.

Alisema kwa mda mrefu wamekuwa wakishindwa kupata takwimu kamili za makosa ya vitendo vya ukatili dhidi ya makundi hayo kutokana na kukosekana kwa mfumo rahisi wa kuhifadhi taarifa kwani makosa yote yanayoripotiwa polisi yalikuwa yakichanganywa pamoja.

“Mfumo huu  utatuwezesha kuwa na takwimu sahihi wakati wote zinapohitajika, tofauti na kuhifadhi kwenye makaratasi na kwa kuchanganya makosa yote…vifaa hivi vitatumika kwa kazi moja tu yakuhifadhi kumbukumbu ya makosa ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia yanayoripotiwa polisi” alisema Nzuki.

Alisema uwepo kumbukumbu sahihi pia uatwasaidia kujua wapi kuna haja ya kuongeza nguvu na pia kujua aina ya matukio ya ukatili na unyanyasaji yanayofanyika kwa wingi na kuweza kuongeza jitihada zaidi zitakazoweza kupambana nao.

Akikabidhi vifaa hivyo vyenye tahamani ya Milioni 75.7  mwakilishi wa CDF Koshuma Tengete alisema mpango huo utaanzia katika Mkoa wa kipoli wa Tarime Musoma na baadaye nchi nzima.

“Leo tumekabidhi Screen, Kompyuta mpakato ‘Lap top’ na mtambo ambayo tumeipata kwa kushirikiana na Shirika la idadi ya watu duniani (UNFPA) na tunaamini itasaidia kuwa na kumbukumbu sahihi zitakazoweza kupatikana popote zitakapohitajika” alisema Tengete.

Pia alisema katika utendaji kazi wao wanakabiliwa na tatizo la kukosa ushirikiano kutoka kwa wananchi na kuongeza kuwa kwasasa wanafanya kazi watunga sera mbalimbali ikiwamo maofisa jamii ambao watawasaidia kufanya kazi kwa ufanisi.

No comments:

Post a Comment

Pages