February 02, 2017

TIGO YAONGEZA KASI YA KILLI MARATHON

Mkurugenzi wa Mawasiliano kampuni ya Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata Akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Udhamini wa Mashindano ya Kilimanjaro International Marathon
 Wateja wakifurahia huduma za Tigo zilizoboreshwa katika Ofisi za Tigo zilizoko Blue Rock jijini Arusha.


Na Woinde Shizza, Arusha.

Kampuni ya Simu za mkononi ya TIGO imejipanga kunogesha mashindano ya Kilimanjaro International Marathon kupitia udhamini mnono ya mashindano hayo kwa upande wa kilomita 21 ambapo licha ya udhamini huo watahakikisha huduma zote muhimu za kifedha zinapatikana katika mashindano hayo.

Mkurugenzi wa Mawasiliano kampuni ya Tigo Kanda ya Kaskazini,George Lugata  amesema kuwa zaidi ya nchi 45 zinatarajia kushiriki katika mashindano hayo ya kimataifa yanayotarajia kufanyika Februari 26 mwaka huu mjini Moshi mkoa wa Kilimanjaro.

George alisema kuwa kampuni ya Tigo imejipanga kuhakikisha kuwa huduma za Tigo Pesa zinapatikana kwa kipindi chote kwani wameongeza idadi kubwa ya mawakala  wataotoa huduma hizo.

“Ni vyema tukatambua kuwa wateja kutoka mitandao yote nchini wanaweza pia kulipia huduma na bidhaa kutoka katika maduka ya wafanyabiashara wowote jijini Moshi kwenye mabango yaliyoandikwa Lipa kwa Tigopesa” Alisema George

Alisema kuwa katika kipindi chote hicho watatoa huduma zenye ubora wa hali ya juu ili kuhakikisha kuwa wa Washiriki na Watakaohudhuria wanafurahia huduma hizo.

Mkurugenzi huyo amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kushiriki mbio hizo zenye hadhi kubwa kitaifa na kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Pages