February 03, 2017

WABUNGE WANAWAKE WAJUMUIKA KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA UWANJA WA JAMHURI MJINI DODOMA


Naibu Spika wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongea na Wabunge (hawapo pichani) pamoja na Waandishi wa Habari kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya leo katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.

Naibu Waziri, Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (Mb) akiongea na Wabunge wenzake (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya ya miili pamoja na matarajio ya Uzinduzi wa Mazoezi yanayotarajiwa kuzinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo yatatangazwa hivi karibuni.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mhe. Ritta Kabati akiongea na Wabunge wenzake pamoja na Waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya ya miili wakati wa mazoezi ya pamoja kwa Wabunge hao wanawake yaliyofanyika leo 03/02/2017 Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Mbunge wa Jimbo la Ilemela Jijini Mwanza (CCM), Mhe. Angeline Mabula akiongea na Wabunge wenzake pamoja na Waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya ya miili wakati wa mazoezi ya pamoja kwa Wabunge hao wanawake yaliyofanyika leo 03/02/2017 Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Baadhi ya Wabunge wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa wameongozana na Spika wa Bunge (wa pili kushoto) wakifanya mazoezi (Jogging) ikiwa ni sehemu ya kufanya mazoezi ya pamoja kwa ajili ya kuweka sawa miili, mazoezi hayo yamefanyika leo 03/02/2017 katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (wa pili kushoto) akifanya mazoezi ya mwili ikiwa ni sehemu ya ya kuweka sawa mwili, mazoezi hayo yamefanyika leo 03/02/2017 katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.(Picha zote na Benedict Liwenga).

No comments:

Post a Comment

Pages