Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye
umri wa miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys imetumia ndege ya Shirika
la Ndege la Tanzania (ATCL) kutoka Dar es Salaam alfajiri ya leo Machi 26,
mwaka huu na kutua Bukoba mkoani Kagera kwa kambi ya wiki moja.
Serengeti Boys itakuwa kambini Bukoba hadi Aprili
2, mwaka huu ambako inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa
dhidi ya timu vijana ya Burundi kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani
Kagera. Michezo hiyo itafanyika Machi 30, 2017 na kurudiana Aprili mosi, mwaka
huu.
Serengeti Boys ambayo inajiandaa na michuano Afrika
huko Gabon itarejea Dar es Salaam Aprili 2, mwaka huu ambako imepangwa kucheza
na Ghana Aprili 3, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo
utatanguliwa na hafla ya kuagwa kwa kukabidhiwa bendera.
Timu itaelekea Morocco Mei 5, mwaka huu baadaye
itapita Cameroon kwenye kambi ya zaidi ya mwezi mmoja baadaye itakwenda Gabon
katika michuano itakayoanza Mei 14, 2017. Ikiwa Cameroon itacheza mechi mbili
za kimataifa dhidi ya wenyeji kabla ya kwenda kwenye fainali.
Serengeti Boys ni timu ya vijana ambayo imefuzu kwa
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Gabon kuanzia Mei 14,
mwaka huu. Timu hiyo imepangwa Kundi ‘B’ pamoja na mabingwa watetezi Mali,
Niger na Angola. Ina lengo la kurejea na Kombe la Afrika kwa vijana.
La ikitokea imekosa nafasi hiyo angalau ikafika
nusu fainali ambako kwa mafanikio hayo itakuwa tayari ina tiketi mkononi ya
kucheza fainali za Kombe la Dunia huko India, Novemba, mwaka huu.
Kikosi cha Serengeti Boys kinaundwa na
Makipa: Ramadhan Kabwili, Samwel Edward na Kelvin Kayego.
Walinzi: Kibwana Ally Shomari, Nickson
Kibabage, Israel Mwenda, Dickson Job, Ally Msengi, Issa Makamba na Enrick
Vitalis Nkosi.
Viungo: Kelvin Nashon Naftali, Ally Ng’anzi,
Mohamed Rashid, Shaaban Ada, Mathias Juan, Marco Gerald, Abdulhamis Suleiman,
Saidi Mussa na Cyprian Benedictor Mtesigwa.
Washambuliaji: Muhsin Malima Makame, Yohana
Mkomola, Ibrahim Abdallah, Assad Juma na Abdul Suleiman.
Benchi la Ufundi:
Bakari Shime (Kocha Mkuu)
Oscar Mirambo (Kocha Msaidizi)
Muharami Mohamed (Kocha wa makipa)
Kim Poulsen (Mshauri wa Ufundi)
Edward Evans (Mtunza Vifaa)
Shecky Mngazija (Daktari wa timu)
No comments:
Post a Comment