NA MWANDISHI
WETU
HATIMAYE
Mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili Boniface Mwaitege, amethibitisha kushiriki
tamasha la Pasaka litakalofanyika April 16 katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar
es Salaam.
Mwaitege aliyewahi
kutamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo Utamtambuaje kama ameokoka, Mama ni Mama
na nyingine nyingi matata, atapanda jukwaani siku hiyo pamoja na waimbaji
wengine wa ndani na nje.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama alisema jana kuwa, Mwaitege
amethibitisha pamoja na Upendo Kilajiro, mmoja wa waimbaji mahiri wa kike
nchini.
Alisema kwa
waimbaji wa ndani, hao ndio wa mwisho tayari kushirikiana na wengine waliotajwa
awali akiwemo malkia wa muziki wa injili Afrika Mashariki na Kati, Rose
Muhando, Martha Mwaipata na Jesca ‘BM na Kinondoni Revival Choir’.
Msama
aliitaja pia kwaya ya Vijana KKKT ya Tabata ambayo itatumbuiza katika tamasha
hilo na kusema ni katika kutoa nafasi kwa kwaya chipukizi kupata uzoefu zaidi
katika huduma hiyo.
Katika hatua
nyingine, Msama alisema awali, baada ya uzinduzi wa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar
es Salaam, uhindo huo ulikuwa uende Uwanja wa Jamhuri, mkoani Dodoma, lakini
sasa hawatakwenda mkoani huko.
Alisema
ingawa Kamati yake ilipenda wadau wa mkoa huo wapate uhondo wa tukio hilo,
lakini hawatakwenda huko kutokana na kukosa nafasi kwa siku ambayo wangekuwa
huko.
Kwa
mabadikilo hayo, Msama alisema baada ya tamasha hilo kutikiza katika Uwanja wa
Uhuru, jijini Dar es Salaam, April 22
itakuwa zamu ya wadau na wapendwa wa Simiyu na siku April 23, itakuwa zamu ya
wadau wa Mwanza.
Alisema
wakiwa jijini Mwanza, tukio hilo litafanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba
ambapo mgeni atakuwa Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Angelina
Mabula.
No comments:
Post a Comment