Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa, akizungumza katika hafla ya chakula jioni kilichoandaliwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 nyumbani kwake Oysterbay. Timu hiyo imeondoka leo kwenda nchini Morocco kuweka kambi ya kujiandaa na Fainali za Afrika zitakazofanyika Gabon. (Picha na Francis Dande).
Nahodha wa timu ya taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya miaka 17, Issa Abdi Makamba, akizungumza katika hafla ya chakula jioni kilichoandaliwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan nyumbani kwake Oyster bay.Timu hiyo imekwenda nchini Morocco kuweka kambi ya kujiandaa na fainali za Afrika zitakazofanyika Gabon.
Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni, Rashid Ally Juma, akizungumza katika hafla hiyo.
Wachezaji wa Serengeti Boys wakiwa katika hafla hiyo.
Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, akizungumza katika hafla hiyo.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akizungumza katika hafla ya chakula jioni kilichoandaliwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan nyumbani kwake Oyster bay.Timu hiyo imekwenda nchini Morocco kuweka kambi ya kujiandaa na fainali za Afrika.
Wachezaji wa Serengeti Boys.
Wachezaji wa Serengeti Boys.
Wachezaji wa Serengeti Boys.
Wachezaji wa Serengeti Boys.
Nahodha wa timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania 'serengeti Boys'chini ya miaka 17, Issa Abdi Makamba, akipokea chakula kutoka kwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan nyumbani kwake Oysterbay wakati wa hafla ya chakula cha jioni alichowaandalia wachezaji wa timu hiyo inayojiandaa na michuano ya fainali za Afrika zitakazofanyika Gabon.
Nahodha wa timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania 'serengeti Boys'chini ya miaka 17, Issa Abdi Makamba, akipokea chakula kutoka kwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan nyumbani kwake Oysterbay wakati wa hafla ya chakula cha jioni alichowaandalia wachezaji wa timu hiyo inayojiandaa na michuano ya fainali za Afrika zitakazofanyika Gabon.
Mshambuliaji wa Serengeti Boys, Abdul Khamis, akipewa chakula na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa hafla ya chakula cha jioni alichowaandaliwa wachezaji hao.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akimhudumia Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.
Wachezaji wakipata chakula cha jioni.
Wachezaji wakipata chakula cha jioni.
Wachezaji wakipata chakula cha jioni.
Wachezaji wakipata chakula cha jioni.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Happi, akizungumza katika hafla hiyo.
Makamu wa Rais akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Serengeti Boys pamoja na viongozi wao.
Makamu wa Rais akiwa katika picha ya pamoja.
NA MAKUBURI ALLY
MAKAMU wa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imelipokea suala la mvutano wa limbikizo la mapato ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusu limbikizo la deni inalodaiwa.
Hatua ya limbikizo la deni ilitoa sura mpya pale, Wakala wa TRA, Kampuni ya udalali ya Yono ilipolikamata basi la timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17, ‘Serengeti Boys’ na kuwashusha wachezaji waliokuwa wanakwenda nyumbani kwa Makamu wa Rais kwenye hafla ya chakula cha usiku iliyofanyika nyumbani kwake.
Akizungumza juzi, nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam, Samia alisema kwa kuwa yaliyotokea yanaihusu Serikali watayafanyia kazi ili kumalizana na suala hilo ambalo halina sura nzuri.
Samia alisema pamoja na serikali kulifanyia kazi suala hilo alitoa wito kwa TFF, kujifunza kulipa kwa wakati ili kukwepa misuguano kama hiyo ambayo inachafua taswira yake .
“TFF mjifunze kulipa kwa wakati kukwepa misuguano ambayo haiendani na michezo, lakini suala lao tunaweza kulitekeleza na kulimaliza,” alisema Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Samia aliwaasa vijana hao kutokucheza soka la miujiza kama ilivyotokea kwenye mchezo kati yao na timu ya Taifa ya Ghana Black Starlets uliochezwa mwanzoni mwa wiki hii na kutoka sare ya kufungana mabao 2-2 ambako alisema wasicheze soka la miujiza na wanatakiwa kucheza soka ndani ya dakika 90.
“Napongeza matokeo ya mchezo kati yenu na Ghana, msicheze kwa miujiza, chezeni ndani ya dakika 90, msiseme watachoka, katika mchezo wa juzi, upuuzi wao wa kujiangusha kila mara ndio uliwapa ushindi,” alisema Mama Samia.
Samia alisema Serengeti Boys wanatakiwa kwenda katika mashindano hayo kushindana na si kushiriki ambako alisema inatakiwa waingie kwenye nne bora ambazo zitakwenda katika fainali ikiwa ya kwanza ama ya pili.
“Serengeti Boys inatakiwa kwenda kushindana na si kushiriki, inatakiwa isiwe katika nafasi ya nne ama ya tatu inatakiwa kuwa ya kwanza ama ya pili lakini isitamkwe kwamba ya kwanza ni halafu inamaliziwa ‘na’ hiyo sitaki,” alisema Samia.
Alisema iwapo Serengeti Boys itafanya vizuri katika michuano ya Afrika inayotarajia kufanyika Gabon ahadi yake hataki kuiweka bayana ili vijana hao wapambane vilivyo ingawa aliwaahidi kuwaandalia hafla maalum nyum,bani kwa Makamu wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd.
Makamu wa Rais alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana hao wasiige kujichora mwilini, kusuka nywele kama ilivyo kwa wachezaji wanaotamba katika soka Kimataifa na kuwataka kuwa katika maisha ya kawaida ili waendane na utamaduni wa Tanzania.
“Vijana mnatakiwa msiige ya kwenye TV kama kusuka nywele, kujichora mwilini wawe kawaida na kulinda utamaduni wa Kitanzania,” alisema.
Aidha Samia Suluhu aliwataka viongozi wa timu hiyo kuwatunza vijana hao na kuwapa matunzo bora, hamasa, upendo ili kuwaendeleza vijana hao kimaendeleo.
Alisema hatutegemei kusikia lolote kwani wamewapa mzigo ambao unatakiwa ufike na ufanye vizuri katika mashindano hayo na kurudi na ubingwa wa Dunia.
Alitumia fursa hiyo kuitaka Kamati ya Hamasa ya timu hiyo inayoongozwa na Mtangazaji nguli, Charles Hillary kujadiliana na kampuni za simu kuwakata wateja kiasi kidogo cha fedha ili kuichangia timu hiyo, alisema pia kamati ingekuwa na akaunti maalum ya benki ili kuwavuta na walioko nje ya Tanzania.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe alisema amesikitishwa na tukio lililofanywa na TRA iliyolikamata basi lililokwenda kuwachukua wachezaji wa Serengeti na kueleza ilitakiwa itumike busara katika kudai deni hilo.
Dk. Mwakyembe alisema ili suala hilo limalizike kwa taratibu, aliwaomba Katibu Mkuu wake, Katibu Mkuu wa Wizaa ya Fedha na Mkurugenzi wa TRA kujadili namna ya kumalizana na deni hilo.
“Nimesikitishwa sana na tukio lile, vijana wako kwenye kampeni ya Kitaifa, deni lenyewe ni aibu kwani ni udhaifu uliofanywa na sisi wenyewe serikali, naomba Makatibu na Mkurugenzi waketi kwa pamoja ndani ya siku mbili hizi na kama ikishindikana, suala hili nitakushitakia Makamu wa Rais,” alisema Dk. Mwakyembe.
Aidha Dk. Mwakyembe alisema alichokifanya Makamu wa Rais ni zawadi kubwa kwa vijana hao baada ya kazi kubwa waliyoifanya katika mchezo dhidi yao na Ghana.
Dk. Mwakyembe alisema Makamu wa Rais amegusa nyoyo za vijana hao kwa kuwaandalia hafla hiyo maalum kwa ajili yao ambayo ni historia ya maisha yao ambacho kimewatia moyo zaidi.
“Serengeti imecheza mechi zaidi ya 12 na zote imefanya vizuri, imeifunga nchi kama Misri ambayo ni tishio katika medani ya soka Afrika, imewafunga Shelisheli mabao 9, nawapa pongezi zaidi vijana wafanye vizuri zaidi katika mashindano hayo,” alisema.
Waziri huyo alisema atahakikisha timu hiyo wanaitunza timu hiyo na mawakala ‘uchwara’ ambao watabomoa mipangilio ya Tanzania kusonga mbele zaidi Kimataifa kupitia wachezaji hao na kuwarubuni kwamba watawapeleka katika timu za ajabu.
Waziri wa Habari wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rashid Ali Juma alisema ana hamasa kubwa kwa vijana hao ambaye aliwaombea dua ambayo itawasaidia kubeba ubingwa wa Afrika na Dunia.
Waziri Juma alisema vijana waende Gabon wakiwa na mawazo kwamba wakirejea na kombe atawaandalia hafla maalum katika ufukwe wa bahari ya Hindi, Zanzibar ambako atagharamia safari na burudani zote kisiwani humo.
Nahodha wa Serengeti, Issa Abdi alisema wanakwenda Gabon kwa ajili ya nchi yetu na wanakwenda kuipigania Tanzania na wana malengo ya kufika fainali ya mashindano ya Afrika na kueleza kwamba wanatamani mwaliko mwingine kwa Makamu wa Rais.
Katika hatua nyingine Kampuni ya udalali ya Yono, juzi usiku ilitangaza kuliachia basi hilo lililokuwa likitumiwa na Serengeti Boys ambao walimtaka Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alifuate basi hilo usiku.
Kwa mujibu wa Lucas basi hilo walilifuata asubuhi ya jana kwa ajili ya kusaidia kuwapeleka vijana hao uwanja wa ndege kwa ajili ya safari yao ya Morocco kuweka kambi ya mwezi mmoja kabla ya kuelekea Gabon kwenye mashindano ya vijana ya Afrika.
No comments:
Post a Comment