May 23, 2017

PBZ, TADB KUWAINUA WAKULIMA VISIWANI ZANZIBAR

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ipo kwenye mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) yanayolenga kuwanufainisha wakulima visiwani Zanzibar kwa kuwapati mikopo ya gharama nafuu ili kuongeza tija katika kilimo visiwani humo.
Wakizungumza katika mkutano wa pamoja wenye lengo la kujadiliana namna bora za kushirikiana katika kumkomboa mkulima mdogo visiwani humo, watendaji wakuu wa taasisi hizo wamesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa sekta ya kilimo na mkazo wa serikali za katika kuwaongezea kipato wananchi wanaojishughulisha katika kilimo; Benki hizo zinapanga kuchagiza hupatikanaji wa fedha za gharama nafuu kwa wakulima hao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ, Bw. Juma Ameir amesema kuwa Benki yake inatambua umuhimu wa kilimo nchini hivyo ipo tayari kushirikiana na TADB ili kuweza kutimiza malengo la serikali ya kuwakwamua katika umaskini wa kipato wakulima nchini.
Naye, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema ushirikiano na PBZ utachagiza kuhamasisha mabenki na taasisi nyingine za kifedha kutoa fedha kwenye mnyororo mzima wa kilimo ili kusaidia mapinduzi katika ya kilimo kwa wakulima visiwani humo.
Makubaliano hayo yanalenga kuitumia PBZ kama mdau atakayetumika kusimamia fedha zenye masharti nafuu na endelevu kutoka TADB na wadau wengine ili kuinua ushiriki wa wakulima wadogo katika mfumo wa kifedha visiwani humo.

No comments:

Post a Comment

Pages