June 13, 2017

MKURUGENZI MANISPAA YA UBUNGO KUJENGA MADARASA MATANO MAPYA SHULE YA MSINGI HONDOGO

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza jambo mara baada ya kuzuru kwa ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (kushoto) na Afisa Uchumi Mkuu Ndg Yamo Wambura wakikagua majengo ya shule ya msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba wakati wa ziara ya kikazi
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii mara baada ya kuzuru kwa ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi  Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua maendeleo ya wanafunzi wa darasa la nne mara baada ya kuzuru kwa ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi  Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayomboakimsikiliza kwa makini Mwalimu Magreth Kapinga mara baada ya kuzuru kwa ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi  Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba
Madarasa manne yaliyoamuliwa kuvunjwa na kujengwa upya madarasa mengine matano katika Shule ya Msingi Hondogo Jijini Dar es salaam
Mwalimu Happness Mashimba akiwa darasani akifundisha somo la Kiswahili darasa la nne kwa kujitolea kipindi hiki cha likizo kama alivyokutwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akifurahia jambo na wanafunzi mara baada ya kuzuru kwa ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi  Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akitoa maelekezo ya kazi mara baada ya kuzuru kwa ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi  Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Leo June 13, 2016 amefanya ziara ya kikazi kwa kutembelea shule ya Msingi Hondogo iliyopo katika Kata ya Kibamba Jijini Dar es salaam kujionea hali ya Miundombinu ikiwemo majengo ya shule na ufanisi wa utoaji elimu katika Shule hiyo.


Mara baada ya kuzuru katika Shule hiyo Mkurugenzi Kayombo amebaini kuwapo na ubovu wa madarasa hivyo kuamua kujenga madarasa mengine mapya matano kwa ajili ya wanafunzi kujisomea kwa uhuru na amani shuleni hapo.



Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa ujenzi huo utakaoanza hivi karibuni wa vyumba vitano vya madarasa utaakisi pia ujenzi wa vyumba vya madarasa nane na matundu ya vyoo katika Shule  ya Msingi Ubungo Plaza, vivyo hivyo katika Shule ya Msingi Kawawa na Shule ya Sekondari  Mburahati ambapo kote huko ameelekeza kuanza haraka ujenzi wa Madarasa  sambamba na Vyoo kwa ajili ya wanafunzi na walimu.



MD Kayombo alisema kuwa mara baada ya kukamilika kwa madarasa hayo  yatapunguza kadhia ya mbanano wa wanafunzi darasani ambapo pia  amesema ujenzi wa madarasa hayo utakuwa wa kisasa ili kukidhi mahitaji ya ubora wa majengo ya serikali.

No comments:

Post a Comment

Pages