Na Talib Ussi, Zanzibar
Wakati Dunia ikijitayarisha kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani, Zanzibar imepata ghofu ya kuongezeka maradhi ya mripuko, kutokana na uharibifu mkubwa wa Mazingira
Jumuiya ya kupambana na mabadiliko ya tabianch ZACCA imesema visiwa vya Zanzibar vinakabiliwa na mabadiliko ya tabianch yatayosababisha upoteaji wa misiti ya asili,kuongezeka kwa maradhi ya miripuko na kupotea kwa rasilimali ya mchanga.
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Amina Yussuf Kashorowa akizungumza na Waandishi wa habari ikiwa ni shamrashamra ya kuadhimisha Siku ya mazingira duniani ambayo kwa Tanzania inatarajiwa kuadhimisha tarehe 5 huko Musoma Butiama.
Aliahamisha kuwa uharibifu wa mazingira unapelekea kuongeza kasi ya athari za mabadiliko ya tabianchi ikiwemo uchimbaji mchanga,ukataji misitu kwa matumizi ya mkaa na kuni,uharibifu wa vyanzo vya maji ikiwemo ujenzi na ulimaji katika maeneo ya vyanzo vya maji na kusababisha mafuriko.
Hata hivyo Amina alieleza licha yajuhudi mbalimbali zinazochukuliwa kupambana na matatizo hayo lakini bado yanashika kasi na kuhatarisha mustakabali wa zanzibar kimazingira.
Aidha alieleza kwamba ni wakati muafaka kwa jamii kuwa na uelewa juu ya tatizo hilo na kutafuta njia bora za kilimo na ufugaji kwani mabadiliko hayo yameathiri sana mifumo ya maisha ikiwemo kilimo,ufugaji,nishati,utalii pamoja na afya.
Aidha Zacca imeishauri Wizara ya fedha ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kutenga fedha zaidi kusaidi miradi ya jamii ya kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi ili kupunguza kasi kwa jamii kuharibu mazingira kama ukataji miti ovyoo kwaajili ya mahitaji yao.
Mwenyekiti huyo alieleza ya kuwa ipo haja SMZ kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kuweka nguvu zao katika kuwaelimisha jamii juu ya athari hizo kwani tafiti zilizofavywa na idara ya misitu na maliasili zisizorejesheka inaonesha Zanzibar inapoteza hekta 500 kwa kila mwaka kutokana wananchi wa Zanzibar wanategemea kuni na mkaa kwa asilimia 97.
No comments:
Post a Comment