Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba (kushoto), akizungumza na maofisa wa Benki ya Kilimo juu ya umuhimu wa kuharakisha utoaji wa mikopo kwa wasindikaji wa maziwa nchini. (Na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu, Bukoba
Waziri
mwenye dhamana ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Charles Tizeba ameiagiza
Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) kuharakisha kutoa mikopo kwa
wasindikaji wa maziwa nchi ili kuongeza tija kwa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa
nchini.
Waziri
Dkt. Tizeba alitoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi wa Benki hiyo
katika Kilele cha Maadhimisho ya Kampeni ya Wiki ya Maziwa iliyokuwa ikifanyika
Kitaifa mjini Bukoba, mkoani Kagera tangu tarehe 28 Mei na kufikia kilele chake
tarehe 01 Juni, 2017.
Dkt.
Tizeba alisema utoaji wa mikopo kwa wasindikaji una umuhimu wa kipekee kwa kuwa
utachangia uhakika wa masoko kwa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa nchini hali
itakayochochea tija kwa wafugaji hao hivyo kuchagiza lengo la Serikali la Awamu
ya Tano ya kuwawezesha wakulima, wafugaji na wavuvi kuweza kunufaika na sekta
hizo.
“Serikali
ya Awamu ya Tano imedhamiria kuwasaidia wakulima, wafugaji na wavuvi hivyo
uanzishwaji wa Benki ya Kilimo lazima usaidie katika kuhakikisha wasindikaji wa
maziwa wanapata huduma za TADB kwa wakati ili tupate uhakika wa masoko kwa
wafugaji wetu ili tuiinue Tasnia ya Maziwa ili ichangie ukuaji wa uchumi na
maendeleo nchini,” alisema.
Kwa
mujibu wa mpango kazi wa TADB, sekta ya mifugo ni mojawapo ya
minyororo ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao
na mifugo mbalimbali hasa katika uongezaji wa thamani wa ufugaji wa ng’ombe wa
nyama na maziwa nchini. Na Benki imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa
Ufugaji wa Ng’ombe wa Nyama na Maziwa ili kuongeza tija kwenye Tasnia za nyama
na maziwa ili kuchagiza maendeleo katika tasnia hizo.
Katika kuhakikisha wasindikaji wa maziwa
wananufaika na huduma za TADB, Benki hiyo inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni
Mikopo ya Muda Mfupi (Hadi Miaka Miwili (2)), Mikopo ya Muda wa Kati (Zaidi ya
Miaka 2 hadi Miaka Mitano (5)) na Mikopo ya Muda Mrefu (Zaidi ya Miaka 5 hadi
Miaka Kumi na Mitano (15)).
Kwa mujibu wa
Mpango Kazi huo, mikopo hiyo ni ya riba nafuu ambayo inalenga katika kuchagiza
na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka
kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa
uchumi na kupunguza umaskini.
TADB ni
taasisi ya serikali ambayo ilianzishwa kwa ajili ya kutatua ufinyu mkubwa wa
upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini ambao
ulikuwa unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha
kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa; riba kubwa kwenye mikopo
ya kilimo; mikopo ya muda mfupi; masharti magumu ya kukopa bila kuzingatia hali
halisi ya sekta ya kilimo na mazao
ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
No comments:
Post a Comment