August 31, 2017

MAMIA WAMIMINIKA KUJISAJILI KATIKA MFUKO WA FIDIA (WCF) IKIWA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA WAZIRI JENISTA MHAGAMA

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MUITIKIO wa waajiri kujisajili na kulipa michango katika Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) umekuwa wa kuridhisha hususani Mwezi Agosti, Meneja Matekelezo Bw. Victor Luvena amesema leo Agosti 31, 2017.

Itakumbukwa ya kwamba, tarehe 23 Julai 2017 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), alitoa siku 30 kwa waajiri wote nchini ambao walikuwa hawajasajili kuhakikisha wanajisajili katika Mfuko na wanawasilisha michango kwa wakati, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao na kama Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi inavyoelekeza.

“Kwakweli tunamshukuru Mheshimiwa Waziri kwa agizo alilolitoa kwani limetoa msukumo mkubwa, waajiri wengi wamejitokeza kutekeleza wajibu wao wa kisheria wa kujisajili na kuwasilisha michango katika Mfuko.” Alisema Bw. Luvena

K-VIS Blog ilishuhudia idadi kubwa ya waajiri wakiwa wamejitokeza leo Agosti 31, 2017 ambayo ndiyo siku ya mwisho kwa waajiri kutekeleza agizo la Mheshimiwa waziri, wakiwa wamejazana kwenye ofisi za WCF kujisajili na kuwasilisha michango, ambapo kazi hiyo ya kuwahudumia ilikuwa ikiongozwa na Meneja Matekelezo - WCF, Bw.Victor Ruvena.

Waajiri, wakihudumiwa na maafisa wa WCF, leo Agosti 31, 2017.

Afisa Matekelezo wa WCF, Bi. Gladness Madembwe, (kulia), akimkabidhi cheti cha usajili Bw.Sultani Ali kutoka kampuni ya Marifas Refregerator ya jijini Dar es Salaam.

Afisa Matekelezo wa WCF, Bw.Edward Kerenge, (kushoto), akiwahudumia waajiri waliofika kujisajili na Mfuko leo Agosti 31, 2017.

Afisa Matekelezo wa WCF, Bw.Edward Kerenge, (kulia), akiwahudumia waajiri waliofika kujisajili na Mfuko leo Agosti 31, 2017.

Afisa Matekelezo Msaidizi wa WCF, Bi.Emiliana J.Gwagilo, (kushoto), akimuhudumia Mwajiri huyu aliyefika kupatiwa huduma leo Agosti 31, 2017.

Afisa Matekelezo wa WCF, Bi. Gladness Madembwe,(kushoto), akimuhudumia Bw. Sultani Ali kutoka kampuni ya Marifas Refrigeration, ya jijini Dar es Salaam.

Meneja Matekelezo Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw.Victor Luvena, (kulia), akiwasikiliza waajiri waliofika leo Agosti 31, 2017 ili kupatiwa huduma ya usajili na uwasilishaji michango katika Mfuko huo.

Maafisa wa WCF (kulia), wakimsikiliza Mama huyu mwajiri aliyefika kupatiwa huduma.

No comments:

Post a Comment

Pages