September 29, 2017

Airtel yatoa mafunzo ya TEHAMA kwa Walimu Dar

Meneja Matukio wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (kushoto) akiangalia namna walimu wa Shule ya Msingi Kijitonyama wanavyojifunza kompyuta katika maabara ya “Airtel Fursa Lab” Dar es Salaam.
Meneja Matukio wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (kushoto) akiangalia namna walimu wa Shule ya Msingi Kijitonyama wanavyojifunza kompyuta katika maabara ya “Airtel Fursa Lab” Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akiangalia namna walimu wa Shule ya Msingi Kijitonyama wanavyojifunza kompyuta katika maabara ya “Airtel Fursa Lab” Dar es Salaam. 

Dar es Salaam, Tanzania
 
Kampuni yasimu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi)  imeanza kutoa mafunzo ya Tehama kwa waalimu katika maabara ya kompyuta iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama Manispaa ya Kinondoni.

Mafunzo hayo kwa waalimu yameanza kufuatia Airtel na DTBi kutangaza kuanza kwa mafunzo hayo na kuwaalika vijana kuanzia ngazi ya shule za msingi,sekondari, vyuo vikuu na wafanya biashara kujiandikisha na kufaidika na mafunzo haya yatakayowasaidia kuvumbua application mbalimbali, kuwapatia vijana ujuzi katika mswala ya Tehama na pia kuwawezesha vijana wajasiriamali kuendesha shughuli zao za kibiashara kwa kutumia technologia za kisasa

Akiongea kuhusu kuanza kwa mafunzo hayo, Meneja Mradi wa Airtel Bi Jane Matinde alisema,
‘Hapo awali tulikuwa tumeanza kutoa mafunzo ya Tehama kwa wanafunzi lakini tumeona ni bora na waalimu wa hapa shule hii Kijitonyama nao waanze kupata mafunzo. Hii itasaidia kwani kwa baadae ndio watakaokuwa wakitoa mafunzo kwa wanafunzi na hii itatupa nafasi ya kuendelea kuwezesha shule zingine.
Waalimu wamepokea hatua hii kwa furaha na wanao hamasa kubwa kwenye mafunzo. Hii inathibitisha nia ya kampuni ya Airtel ya kutoa fursa kwa kila Mtanzania, aliongeza Matinde.
Hata hivyo, Matinde alisema kuwa mafunzo kwa wanafunzo ambao walikuwa washaanza yataendelea vile vile. ‘Utaratibu wa kutoa mafunzo kwa wale wanafunzi ambao walikuwa washaanza utaendelea vile vile. Kilichofanyika ni chukua hatua ya ziada ya kuwapa walimu mafunzo ya Tehama ili nao waweze kuwa kwenye nafasi ya kutoa mafunzo kwa wanafunzi hawa’ alisema Matinde.

Matinde aliongeza kuwa bado tunapokea maombi ya kujiunga hivyo tunatoa wito kwa vijana wa sekondari , wale waliomaliza darasa la saba , wafanyabiashara kutumia vyema maabara hii yenye lengo la kuwezesha jamii  hususani vijana kuongeza ujuzi na ueledi kwenye maswala ya technologia na Tehama kwa ujumla.

Kwa upande wake Meneja wa maabara ya Airtel Fursa, Agape Jengela alisema “ Tayari tumejipanga kutoa mafunzo kwa walimu wa shule ya Kijitonyama. Tuhahakisha kuwa walimu wamepata mafunzo na kuelewa kabisa ili nao waanze kutoa mafunzo na elimu kwa wanafunzi.

Jengela alisema mafunzo hayo ni pamoja na lego Robotics, program za uhuishaji kwa watoto(ziitwazo scratch) na ubunifu na uchapishaji wa“3D objects”  msingi wa kompyuta, uelewa wa kompyuta, kutengeneza program mbali mbali

Bado tunapokea maombi,   Tunato wito kwa wazazi na walezi kuwaandikisha vijana wao kwa kupitia  www.teknohama.or.tz na  www.airtelfursa.com  au kwa kutembelea maabara  iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama

No comments:

Post a Comment

Pages