September 25, 2017

CRDB yamwaga Mil.100/- ujenzi ofisi za walimu Dar

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, wakati wa kukabidhi mchango wa Sh. Mil. 100 uliotolewa na benki hiyo kwa ajili ya Ujenzi wa Ofisi za Waalimu Dar es Salaam.

Mkurungenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akimkabidhi Mkuu wa  Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mfano wa hundi ya Sh. Mil. 100 kwa ajili ya Ujenzi wa ofisini za waalimu jijini humo. Kushoto  ni Mkurugenzi Wa Masoko na Utafiti na Huduma kwa Wateja wa benki ya hiyo, Tully Mwambapa na Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi wa ofisi za waalimu, Kanali Charles Mbuge.
Mkurungenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akibadilishana mawazo na Mkuu wa  Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. 
Mkurungenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akibadilishana mawazo na Mkuu wa  Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi wa ofisi za waalimu, Kanali Charles Mbuge.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akimkabidhi hundi halisi ya Sh. Mil. 100 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
 Picha ya pamoja.
 
NA FRANCIS DANDE

BENKI ya CRDB, leo imekabidhi hundi ya shilingi milioni 100 kwa uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 40 vya ofisi za waalimu katika mkakati wa kuinua na kuboresha kiwango cha elimu.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi hundi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei alisema huo ni mwendelezo wa misaada yao kwa sekta ya elimu kwani wamewahi kuchangia ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu, maktaba, matundu ya vyoo, vitabu na vifaa vya kufundishia.

Dk. Kimei alisema wao wanajivunia kuwa miongoni mwa wadau wa maendeleo ya elimu nchini mbali ya kufayafanya hayo kwa mwaka 2016, ndani ya mwaka huu wa 2017, wametumia zaidi ya shilingi mil 300 katika ufadhili ujenzi wa majengo ya madarasa katika shule mbalimbali nchini.
Alizitaja shule zilizowahi kunufaika ni shule ya msingi Msasani na Uhuru Mchanganyiko za jijini Dar es Salaam, shule ya Msingi Boma  na Usa River za Arusha pamoja na shule ya msingi Ruangwa ya mkoani Lindi.

“Tunajivunia kuwa miongoni mwa wadau wakubwa wa maendeleo ya elimu nchini ambapo kwa mwaka 2017 pekee, tumetumia zaidi ya shilingi mil 300 katika ufadhili wa majengo ya madarasa katika shule mbalimbali nchini,” alisema Dk. Kimei.

Kuhusu msaada huo wa shilingi mil 100, Dk. Kimei alisema wanaamini utafanikisha ununuzi wa jumla ya mifuko 10,000 ya saruji ambayo itawezesha kujenga vyumba vya ofisi 40 katika mkoa wa Dar es Salaam.
“Kwa kifupi, benki ya CRDB inajitolea kujenga majengo 40 ya ofisi za walimu wa mkoa wa Dar es Salaam,” alisema Dk. Kimei.

Kwa upande wa uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam, umeshukuru kwa msaada na kuipongeza benki hiyo kwa kuendelea kuwa mdau mkubwa katika maendeleo ya  wananchi kwa kujali mahitaji yao muhimu.

No comments:

Post a Comment

Pages