September 01, 2017

MAAFISA WA WIZARA YA USHIRIKIANO WA MAENDELEO YA UJERUMANI WATEMBELEA MAHAKAMA YA AFRIKA


Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR)Sukhdev Chatbar(kulia)akiwaongoza wageni kutoka Wizara ya ushirikiano wa maendeleo ya Ujerumani kupitia taasisi zake GIZ na AGA waliotembelea mahakama hiyo wamekua ni wadau wakubwa katika kusaidia miradi mbalimbali ya mahakama hiyo.

Mkutubi wa Maktaba ya mahakama hiyo,Revina Moshi akizungumza na maafisa kutoka shirika la maendeleo ya kimataifa ya Ujerumani(GIZ),kutoka kushoto ni Afisa wa Wizara ya maendeleo ya Ujerumani anayehusika na Umoja wa Afrika(AU) ofisi ya Addis Ababa,Ethiopia,Barbara Schaefer,Janina Hasse kutoka Berlin,Mkuu wa taasisi za GIZ na AGA,Hartmut Krebs

Mkuu wa taasisi za GIZ na AGA,Hartmut Krebs akiangalia sehemu ya machapisho kwenye maktaba ya AfCHPR.

Msajili wa mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR),Dk Robert Enno(kulia)akizungumza na ujumbe kutoka taasisi za Wizara ya maendeleo ya Ujerumani waliotembelea mahakama hiyo.

Msajili wa mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR),Dk Robert Enno akimkabidhi zawadi ofisa wa Wizara ya maendeleo ya Ujerumani anayehusika na Umoja wa Afrika(AU) ofisi ya Ethiopia,Barbara Schaefer.

No comments:

Post a Comment

Pages