September 10, 2017

Maalim Seif ataka mjadala wa kitaifa

Katibu Mkuu wa chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na na Vijana wa chama hicho mara baada ya kufungua mkutano mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A Unguja uliofanyika katika Ofisi ya Wilaya hiyo ilioko Mkokotoni Unguja

Na Talib Ussi, Zanzibar

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad ametoa wito kwa serikali ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania kuandaa mjadala maalumu wa kitaifa ambao utajadili juu suala la uvunjifu wa Amani unaoendelea Nchini.
 
Maalim Seif alitoa wito huo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Vijana wa chama hicho kwa Wilaya Kaskazini A Unguja na kueleza kuwa kutokana na viteno vinavyohatarisha Amani ya Tanzania iko haja kuwepo kwa mjadala mkuu wa kitaifa ambao alipendekeza kushirikishwa watu mbali mbali wakiwemo viongozi wa vyama vya Siasa,
 
“Haiwezekani Maisha ya watanzania yanakuwa hatarini halafu halafu tukae tuu ni lazima Serikali inayongozwa na Rais John Pombe Magufuli ikybali kuweka mjadala wa kitaifa ili kuangalia wapi tumejikwaa” alieleza Maalim Seif.

Alieleza kuwa Tanzania ilikuwa ikitambuliwa kama kisiwa Cha Amani na kudai kuwa vitendo vya kuvamiwa Ofisi za Mawakili na Kupigwa risasi Mbunge ni kuonesha sifa ya Tanzania imepotea.

“Yaani leo Mbunge anapigwa risasi Ovyo, hili haliwezi kukubalika hata siku lazima tuwe na mjadala wa Kitaifa” alisema Maalim Seif.

Alifahamisha kuwa watanzania sasa wamekuwa waoga ndani ya Nchi yao jambo ambalo ni baya katika Taifa ambalo likisifiwa kwa Amani.

Alieleza kuwa kuendelea kwa Vitendo hivyo bila kuchukuliwa hatau ni sawa na kutoa Baraka vitendo hivyo viendelea jambo ambalo alilielezea linatia ghofu na kutishia uchumi wa Nchi.

“Lazima tuwe na juhudi za maksudi na tuzingatie maoni ya watanzania katika kuleta Amani ya na siyo wachache wajifungie na kuwapatia kitu watanzania ambacho hawajaaamua, lazima sote tushiriki katika kupatia njia ya kuinusuri nchi yetu” alieleza Maalim seif ambaye ni Makamu wa Kwanza Mstaafu katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Sambamba na hilo amelitaka Jeshi la Polisi Nchini kuipokea Oda ya Rais wa Jamuhuri katika kulifanyia kazi tukio la kupigwa Risasi Mbunge wa Singida Mashariki kama wanavyozifanyia kazi amri nyengine kutoka juu.
 
“Mara nyingi tunawasikia Jeshi hili likisema hii ni amri kutoka juu, basi na hili Magufuli kasema waliofanya unyama dhidi ya Mbunge wetu lifanyiwe kazi sio Mkubali kuwakamata Wapinzania tuu ambao wapo kikatiba” alieleza Maalim Seif.

Alieelza kuwa kama Jeshi la Polisi wanataka kurudisha Amani kwa raia basi alieleza kuwa ni vyema maharamia wale ambao tayari watu mbali mbali waliwaripoti wakamatwe.

“Ukiligusa Jeshi letu linakuambia linafanyakazi kisayansi, basi tunataka kuiona sayansi yao kwenye kwani ni kitendo ambacho ni cha kinyama sana kwa taifa hili” alieleza Maalm Seif.

Alieleza kuwa Sayansi yao, ifanye kazi ili hao watu waliopewa jina la watu wasiojuilikana wajuilikane kwa maslahi ya taifa.

“Tunaomba uchunguzi huu kisayansi ufanywe kwa haraka kwani taifa limo katika ghofu kubwa” alisema.
 
Alieleza kuwa kitendo alichofanyiwa Tundu Lisu ni cha kinyama, na Kikatili ambacho alidai hakivumiliki katika ulimwengu huu na kama Serikali iliyomakini basi watu wangaikwisha kamatwa.
Alisema kuwa vitendo vimekuwa Vingi bila kuchukuliwa Hatua na kuonekana kana kwamba na mambo ya kawaida akieleza kuvamiwa Redio Clouds, Nape Mnauye, Ofisi za Mawakili IMMA, na kupigwa Risasi Tundulisu, ili kuondoa dhana hiyo basi tunataka kuona nhatua zimechukuliwa.

“Tatizo la Serikali hii haitaki kukosolewa jambo ambalo limekuwa tofauti na awamu zoote zilizopita kitu ambacho ni kibaya kwa taifa” alieelza Maalim Seif.

No comments:

Post a Comment

Pages