September 02, 2017

MAENDELEO BANK YAWAZAWADIA WATEJA WAKE VIWANJA ,MABATI NA SARUJI

Mkuu wa Tehama na Uendeshaji Bw. George Wandwalo akibonyeza kitufe kuashiria kuanza kwa droo iliyomuibua mshindi wa kiwanja Bi. Dora Olotu katika droo iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bw. Bakari Maggid
Mkuu wa Tehama na Uendeshaji Bw. George Wandwalo akizungumza na mteja wa Maendeleo Bank kwa njia ya simu baada ya kuibuka kama mmoja wa washindi waliopatikana katika droo iliyoashiria kumalizika kwa awamu ya kwanza ya promosheni ya Maendeleo Pamoja na Wewe.C:\Users\EAG Group\Desktop\PRESS MAENDELEO BANK AUG 31 2017\1T4A9121.JPG
Mkuu wa Kitengo cha Fedha Bw. Peter Tarimo akizungumza na waandishi wa habari juu ya shindano na promosheni ya Maendeleo Pamoja na Wewe kabla ya kuanza kwa droo hiyo Dar es Salaam leo.
Maendeleo Bank leo imechezesha droo yake ya kwanza iliyotokana na kampeni ya Maendeleo Pamoja na Wewe iliyozinduliwa rasmi mwanzoni mwa mwezi Agosti 2017.
Promosheni hiyo ina malengo kadhaa;Kuwaweka wateja wake karibu kwa kutumia huduma mbalimbali za Maendeleo Bank Kuwajengea watanzania utaratibu wa kuweka akiba kwa njia ya kibenkiKukuza utamaduni wa kujiwekea malengo ya muda mfupi na mrefu kwa kuweka fedha kidogo kidogo katika akaunti ya WEKEZA ili kufanikisha malengo yao Kuwajengea wazazi utamaduni wa kuwawekea watoto wao akiba.
Mkuu wa Idara ya Fedha wa benki hiyo Bw. Peter Tarimo alisema “Draw yetu ya Maendeleo Pamoja na Wewe awamu ya kwanza inahitimishwa leo kwa kuchezesha draw ambayo itatupatia washindi mbalimbali ikiwemo tani za simenti, kiwanja, mabati na ada ya shule”.
Draw hiyo imeibua washindi wane (4) ambao walishinda kiwanja, mabati 64 ,tani 3 za simenti pamoja na ada ya shule na kushudiwa na mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini Bw. Bakari Maggid.
Promosheni ya Maendeleo Pamoja na Wewe inasitishwa kwa sasa kupisha zoezi za uuzaji wa hisa za Maendeleo Bank na itaendeleo mara baada ya kuhitimisha uuzaji wa hisa za benki hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages