Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza (kulia) kunisalimia na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa Bi Hana Kibopile alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho ya Utalii yaliyoanza leo kwenye Viwanja vya Kichangani mkoani Firings.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw. Richard Kasesera (kulia) akisalimiana na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa ,Bi Hana Kibopile alipotembelea banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania.
Na Mwandishi Wetu, Iringa
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe kesho atafungua rasmi maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim, yanayofanyika kwenye viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.
Maonesho hayo yenye kaulimbiu ya Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda yanashirika taasisi za serikali, mashirika ya umma na kimataifa zaidi ya 400, ambapo yatamalizika Oktoba 2, 2017, ambapo yanalengo la kuweka uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa utalii na thamani thamani ikiwa ni pamoja na kuutangaza utalii kwa kuihamasisha jamii kutumia fursa za utalii zilizopo katika kuinua uchumi wa wakazi wa Ukanda wa Kusini mwa Tanzania na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wa Wizara mbalimbali zipo na taasisi zake ikiwemo Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Idara ya Utalii, Wanyamapori, Mambo ya Kale na Misitu na Nyuki, Chuo cha Taifa cha Utalii, Makumbusho ya Taifa, Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mamlaka ya Usimamizi ya Wanyamapori (TAWA) Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF).
Taasisi nyingine ni Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, (TFS) Taasisi ya Utafiti wa Misitu na Wadau wa Wizara ya Maliasili na Utalii.Wadau wa Sekta ya Utalii kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini watashiriki kuonesha bidhaa na huduma zao muhimu na mikoa inayoshiriki ni pamoja na wenyeji Iringa, Mbeya, Ruvuma, Songwe na Njombe.
Fursa zilizopo nyanda za Juu Kusini ni pamoja na Ziwa Tanganyika, Ziwa Rukwa, Ismila,Kalenga na Boma la Mkuu wa Wilaya, Hifadhi za Mahale, Katavi, Ruaha, Kitulo na Selous.

No comments:
Post a Comment