Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA
Serikali
imedhamiria kununua mashine tatu za vipimo vya vinasaba (DNA) ili
zitumike katika maabara za Kanda na hivyo kusogeza huduma karibu na
wananchi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa
Afya, Maendeo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangala
wakati akijibu swali la Mbunge wa Chumbuni Mhe. Ussy Pondeza kuhusu
ucheleweshwaji wa matokeo ya uchunguzi wa sampuli ikiwemo sampuli za
makosa ya jinai.
Dkt Kigwangala amesema kuwa
Serikali ina mkakati wa kuongeza mashine hizo ili kuwezesha uchunguzi
kufanyika kwa wakati kwa vielelezo vya makosa ya jinai ikiwa ni pamoja
na vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na watoto.
"
Sampuli za uhalali wa watoto kwa wazazi zinafanyika kwa wepesi zaidi
kuliko sampuli za makosa ya jinai kwani sampuli hizo zinachukuliwa moja
kwa moja toka kwa wahusika hivyo kurahisisha uchunguzi wake endapo
wahusika wa uchukuaji watachukua kwa umahiri na uhifadhi utafanyika kwa
namna stahili" amefafanua Dkt. Kigwangala.
Aidha,
Dkt. Kigwangala amesema kuwa sampuli za uchunguzi wa makosa ya jinai
zinachukuliwa toka maeneo ya matukio hivyo uchunguzi wake unaweza
kuchukua muda zaidi kutegemeana na aina ya sampuli na eneo zilipotoka.
Vilevile
Dkt. kigwangala aliongeza kuwa Serikali inampango wa kuanzisha kituo
cha kupima vinasaba (DNA) Mkoani Mbeya kwa lengo la kupunguza
ucheleweshaji wa matokeo ya uchunguzi.
Mbali na
hayo akijibu swali la Mbunge wa Mtwara Vijijini Mhe. Hawa Ghasia kuhusu
Serikali kuagiza tohara kuwa lazima kwa wanaume nchini, Dkt. kigwangala
amesema kuwa si rahisi kwa Serikali kuagiza tohara kuwa lazima japo
kuwa inafaida kiafya kwa wananchi.
" Tohara
inasaidia kupunguza maambukizi ya Saratani ya shingo ya Uzazi kwa
wanawake pamoja na maambukizi ya virusi vya Ukimwi" ameongeza Dkt.
kigwangala.
Aidha, amesema kuwa elimu kuhusu
tohara imefikishwa kwa wananchi kwa kiasi kikubwa ambapo Serikali kwa
kushirikiana na wadau katika Mikoa ya kipaumbele imekuwa ikitoa elimu
kabla na baada ya huduma ya tohara katika vituo vya kutolea huduma za
afya.
No comments:
Post a Comment