.Tigo kuzipatia shule 50
za sekondari nchini vifaa vya elimu vya kidigitali
- Shule tatu mkoani Arusha kuwa za kwanza kunufaika na Mradi wa Tigo wa E-shule
Dar es
Salaam Sept 7, 2017- Kampuni inayoongoza ya kidigitali Tanzania, Tigo Tanzania leo imetangaza
azima kubwa ya kuiweka elimu ya sekondari katika digitali, kwa kutoa vifaa vya
kidigitali vya kujifunzia kwa shule za
sekondari 50 nchini kote kama sehemu ya Tigo Fiesta 2017 – Tumekusomaa sherehe za kitamaduni
zilizopangwa kuburudisha taifa kuanzia wikendi hii.
Kama sehemu ya jitihada zake za Tumekusoma, ambazo zinasisitizia sifa
yenye nguvu kama nembo ya kampuni ya simu ambayo inaelewa vyema na kuitikia
mahitaji ya wateja wake, Tigo itakuwa
inatoa vifaa vya elimu vya kidigitali kwa shule zilizoko katika mikoa 12 kati
ya 15 ambako sherehe za Tigo FIesta 2017 – Tumekusomaa zitakuwa zinafanyika.
Akitoa tangazo kubwa wakati wa makabidhiano
ya vifaa vya kujifunzia katika shule ya Sekondari Arusha jana, Afisa Mkuu wa
Ufundi na Habari (CTIO) Jerome Albou, alisema kwamba azima ya kidigitali
itashuhudia shule zingine 50 za sekondari ambazo mwanzo zilipatiwa computer na
kuunganishwa na mtandao wa internet, pia sasa zinapokea vifaa vya elimu vya
kidigitali kuongeza uwezo wa kujifunza wa wanafunzi na kuwaandaa kuwa sehemu ya
kijiji cha dunia cha kidigitali.
'Tunaishi katika ulimwengu wa kidigitali na
Mradi wa Tigo wa e-shule unawawezesha wanafunzi kuwa sehemu ya ulimwengu wa
kidigitali, 'alisema Albou, wakati akiwa anabainisha jitihada mpya Shule
zingine mkoani Arusha ambazo zimenufaika kutokana na mradi wa e-shule ni Shule
ya Sekondari ya Arusha Day na Shule ya Sekondari Ilbouru.
Mwaka 2016, Tigo iliingia katika ubia na
Wizara ya Mawasiliano, Kazi na Miundombinu kuwezesha ufunguzi wa vituo vya
kuwezesha upatikanaji wa mtandao wa internet katika shule za sekondari nchini
kusaidia mradi wa serikali wa e-shule kwa muda wa miaka 2.
Kama sehemu ya makubaliano, Wizara
ilibainisha na kutoa orodha za shule ambazo hazina vyumba vya computer
viunganishwe na pia kupewa mwongozo wa utekelezaji wa mradi. Tigo ilifadhili
uendelezaji wa miundombinu katika shule nchi nzima, ikiwemo kuunganisha nyaya
madarasani na ufungaji wa LAN zisizotumia waya pamoja na vituo vya kuunganisha
mtandao wa internet. Hatua ya tatu ya mradi huu ni ufungaji wa sasa wa vifaa
vya kujifunzia ambavyo mwanafunzi ataweza kuvipata moja kwa moja kutoka katika
chumba cha computer, hivyo kufanya mtindo wao wa kujifunza kuwa wa kidigitali.
"Kupitia katika
jitihada zetu za uwajibikaji kwa jamii, sasa tunatekeleza dhamira ya serikali
ya kubadilisha nchi kuelekea uchumi wa misingi ya kitaluma kufikia mwaka 2025. Kampini yetu imeazimia kuhakikisha kuwa idadi
kubwa ya shule za sekondari zina huduma ya internet nchini Tanzania, pia vifaa
vya kujifunzia ili waweze kujiandaa
vyema kwajili ya fursa ambazo zinakuja na mabadiliko ya kidigitali ambayo kwa
sasa yanaukabili ulimwengu," Alilsema CTIO wa Tigo.
Alibainisha shule ambazo zitanufaika kutokana na mradi kuwa ni Shule ya Arusha Day, Ilbouru na Shule ya Sekondari ya Arusha katika mkoa wa Arusha; Shule za sekondari za Mwanza, Pamba na Milambo mkoani mwanza; Shule ya wasichana ya Tabora na Milambo mkoani Tabora; na Mpwapwa sekondai mkoani Dodoma.
Nyingine ni shule za sekondari Iringa na
Kleruu mkoani Iringa; Shule ya sekondari Mtalewa na Shule ya sekondari ya
wasichana Songea mkoani Songea; Shule ya sekondari Njombe na Mpechi mkoani
Njombe; Shule ya sekondari Morogoro manispaa na Mzumbe za mkoani Morokogoro; na
Shule ya sekondari Handeni na Shemsanga mkoani Tanga.
Shule zingine
zitakazo nufaika na vifaa vya elimu vya kidigitali vinavyotolewa na Tigo
kupitia e-shule ni, Shule ya sekondari Lyamungo na Shule ya wasichana Machame
Moshi; Shule ya sekondari ya Newala na Masasi katika mkoa wa Mtwara wakati
katika mkoa wa Dar es salaam shule zitakazo nufaika ni pamoja na Mbagala, Kibamba, Benjamini Mkapa na Shule ya
sekondari Makumbusho.
'Tigo inajivunia kuwa mbia na Wizara ya Mawasiliano,
Kazi na Miundombinu na shule kuwawezesha
vijana na jamii kwa ujumla kuweza kubisha hodi katika ulimwengu wa taarifa na
ufahamu, ambako watajifunza, kupanua ubunifu wao na kushirikiana na wenzao
duniani kote', aliongeza Albou.
Mradi wa E-shule ni moja kati ya
mikakati ya miradi ya Tigo ya kuwekeza katika jamii na mpaka sasa Tigo imesha
unganisha katika mtandao wa internet sekondari 60 za umma kutoa computer 77 kwa
sekondari na taasisi za elimu ya juu nchini.
No comments:
Post a Comment