HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 07, 2017

AZANIA BANK ,TAWI LA MOSHI WAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KULA KEKI NA WATEJA WAO

Wafanyakazi wa Azania Bank tawi la Moshi wakikata keki kwa pamoja kwa ajili ya kushiriki na Wateja wao ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja inayoendelea.
Wafanyakazi wa Azania Bank tawi la Moshi wakiwa katika muonekano tofauti ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.
Mfanyakazi wa Azania Bank ,tawi la Moshi ,Aida Mbilinyi akimuelekeza jambo mteja wa Benki hiyo Ibrahim Shoo alipofika katika tawi hilo kwa ajili ya kupata huduma.
Mfanyakazi wa Azania Bank,tawi la Moshi,Asifiwe Musa akiwa ni mwenye tabasamu wakati akitoa huduma kwa mmoja wa wateja wa Benki hiyo waliofika kupata huduma.
Mfanyakazi wa Azania Bank,tawi la Moshi,Diana Ngaiza akimhudumia mmoja wa wateja wa Benki hiyo waliofika kwa ajili ya kupatiwa Huduma za kibenki.
Baadhi ya Wateja wakipata Huduma katika madirisha ya Huduma ndani ya Benki hiyo.
Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi ,Bi Hajira Mmambe akiwalisha keki baadhi ya Wateja waliofika kupata huduma katika Benki hiyo.
Wafanyaazi wa Azania Bank tawi la Moshi wakiwa katika picha ya pamoja nje ya jingo la Benki hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

Pages