Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen
amewatahadharisha wananchi wa Mkoa huo kujihadhari na mvua zilizoanza na upepo ulioezua baadhi ya paa za
nyumba na vituo vya kutolea huduma katika baadhi ya maeneo ya mkoa.
Amesema kuwa sasa ni wakati wa wazazi kuwachunga watoto
katika msimu huu wa mvua na kuongeza kuwa wenye nyumba hawanabudi kuimarisha
majengo yao mapema ili kuepukana na hasara ambayo wangeweza kuipata baada ya
madhara kutokea.
“Ni wakati muafaka hivi sasa kila mtu kuchukua tahadhari
kuangalia watoto, kukagua majengo yetu kuona kuwa yapo imara na pale ambapo
ninatokea basi wajue sehemu salama ya kukimbilia ili kuokoa Maisha,”
Ameyasema hayo aliposhiriki kufanya usafi nyumbani kwake
eneo la Mkoani, mjini Sumbawanga. Ambapo alisema kuwa suala la usafi linaanzia
nyumbani kwa mtu na kuwa wananchi wafanye usafi kwa faida yao wenyewe na
kuendelea kuwasisitiza Wakurugenzi wa Halmashauri kuendelea kusimamia usafi
kuanzia ngazi ya Kijiji au mtaa ili kutekeleza agizo lake la kufanya usafi
kuanzia katika ngazi hizo.
“Nimewaagiza wakurugenzi na wataalamu wake wakague usafi
kwasababu suala la usafi ni faida kwa kila mtu, siyo faida ya rais wa la mkuu
wa mkoa pekee, kwasababu tukiingiliwa na magonjwa halitakuwa la rais peke yake,”
Alisema
Pamoja na hayo Mh. Zelote aliwaonya wenye tabia ya kuchoma
misitu hasa katika kipindi hiki cha kukaribia msimu wa kilimo, hivyo amewasisitiza
viongozi kuanzia ngazi ya Kijiji kushirikiana kuhakikisha kuwa jambo hilo
halijitokezi.
“Katika kipindi hiki uchomaji hovyo wa mioto unaonekana
kushika kasi, ni juu ya serikali ya Kijiji ama kata kuwa mstari wa mbele kuhakikisha
kwamba mioto haiwashwi ovyo ovyo na atakayefanya hivyo achukuliwe hatua za
kisheriakwani mambo haya huaribu mazingira na pia usipodhibitiwa hule madhara,”
Alisisitiza.
No comments:
Post a Comment