Mkurugenzi
wa Kampuni ya Udalali ya Msama, Alex Msama amekishukuru Chama cha Wanamuziki (TAMUNET) na wanamuziki kwa ujumla kwa kutambua
mchango wa kampuni yake na kutambua mchango wake binafsi kutokana na
kazi anayoifanya ili kupunguza kazi haramu za musiki na filamu hapa
nchini.
Msama
ametoa shukurani hizo baada ya kupokea barua kutoka taasisi hiyo
ya muziki ikimpongeza kwa kazi anayoifanya katika kuhakikisha hakuna CD
feki za kazi za muziki na filamu hapa nchini huku , akisisitiza kuwa CD
zote zinatakiwa kuuzwa huku zikiwa na stika za TRA na mtu yeyote
atakayeuza CD zisizo na stika za TRA atakamatwa na kufikishwa katika
vyombo vya sheria, Pitia barua iliyotumwa kutoka chama cha Tanzania
Musicians Network kwenda kwa Msama hapa chini.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Udalali ya Msama, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam baada ya kupokea barua ya pongezi kutoka Chama cha Wanamuziki Tanzania (TAMUNET), Pia Msama alizungumza zoezi la kuwakamata watu wanaojihusisha na wizi wa kazi za wasanii katika eneo la Tegeta.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Msama, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu zoezi la kuwakamata wafanyabiashara wa CD feki pamoja na wale wanaoingiza nyimbo za wasanii katika simu katika maeneo ya Tegeta.
No comments:
Post a Comment