Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Lipuli iliyopangwa kuchezwa Jumapili, Novemba
26, 2017 kwenye Uwanja wa Azam Complex sasa itafanyika kwenye Uwanja wa Uhuru.
Awali
mechi hiyo ilihamishiwa Azam Complex baada ya wamiliki wa Uwanja wa Uhuru kueleza
kuwa utakuwa na matumizi mengine Novemba 26, 2017. Hata hivyo, Novemba 22, 2017
Bodi ya Ligi Kuu ilipokea barua kutoka kwa Mmiliki wa Uwanja wa Uhuru ikieleza kuwa
uwanja wake sasa uko wazi kuwa mwenyeji wa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa
10 jioni.
IMETOLEWA NA BODI YA
LIGI KUU TANZANIA
No comments:
Post a Comment