Mgeni Rasmi katibu Tawala wa Wilaya ya Urambo, Paschal Byemelwa kulia ni Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Urambo Bi.Margareth Nakainga,wapili kutoka kulia ni Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Bw.Gwamaka Mwakilembe,na wa kwanza kushoto ni Meneja wa Tigo mkoa wa Tabora Bw.Bright Kisanga wakipiga makofi kushangilia tukio la kutaka utepe kama ishara ya Uzinduzi wa Duka hilo la Kisasa wilayani Urambo.
Urambo, 12 Desemba, 2017- Katika
mwendelezo wa harakati za kuhakikisha kuwa wateja wake wote wanapata huduma
bora kwa urahisi, kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali Tigo Tanzania
leo imezindua duka kubwa la kisasa wilayani Urambo katika Mkoa wa Tabora.
Duka hilo jipya linapatikana katika mtaa wa Nsanjo,
mkabala na depot ya Pepsi katika mji wa Urambo, lina uwezo wa kuwahudumia
wateja zaidi ya 580,000 wa Tigo wanaopatikana wilayani hapo na viunga vyake.
Akizungumza katika hafla fupi ya kuzindua duka hilo
jipya la Tigo, Meneja wa Eneo la Ziwa wa Tigo, Gwamaka Mwakilembe alisema kuwa
ufunguzi wa duka hilo jipya unaendana na mpango wa upanuzi na ukuaji wa kampuni
hiyo ya simu unaolenga kuongeza idadi ya vituo vya huduma kwa wateja huku
ikihakikisha kuwa bidhaa na huduma zote zinapatikana kwa urahisi na wateja wake
nchi nzima.
‘Tigo imejizatiti kufanya uwekezaji utakaohakikisha
wateja wetu wanapata huduma kwa viwango vya kimataifa ili waweze kupata
suluhisho muafaka kwa mahitaji yao. Ufunguzi wa duka hili la kisasa mjini Urambo
kunafanya idadi ya maduka yetu ya Tigo kufikia 15 katika Ukanda huu wa Ziwa,
huku jumla ya maduka yetu yote ya Tigo nchini ikifikia 75,’ alisema.
‘Uzinduzi huu unaendana na sifa kuu ya Tigo kuwa
mtandao unaowaelewa zaidi wateja wake na kuwapa bidhaa na huduma bora, za
kibunifu, zinazoendana na mahitaji yao. Tunaendelea kuwekeza katika upanuzi na
uboreshaji wa mtandao wetu wa simu, ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anakuwa
sehemu ya mabadiliko na faida za ulimwengu wa kidigitali unaoongozwa na Tigo,’ Mwakilembe
alifafanua.
Kwa
upande wao, wakaazi wa Urambo wameelezea kufurahishwa kwao na ujio wa duka hilo
jipya la Tigo kwani litawapunguzia adha ya kusafiri kwa mwendo mrefu kupata
ufumbuzi wa matatizo yao ya simu pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma za
simu katika wilaya hiyo.
No comments:
Post a Comment