Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Kheri Denice James
akizungumza na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi na Jumuiya zake Wilayani
nzega mkoa wa Tabora.
Na Mwandishi Wetu, Tabora
Umoja
wa Vijana wa CCM umesema umeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi
ya afya inayotokana na ahadi katika ilani ya uchaguzi katika halmshauri
za wilaya mji wa Nzega na Nzega vijijini mkoani Tabora.
Pia
Umoja huo umeeleza kikubwa kasi hiyo inatokana na kuwepo kwa
mashirikiano makubwa kati ya viongozi wa chama,halmashauri za wilaya na
serikali kuu.
Matamshi
hayo yametamkwa jana na Mwenyekiti wa Taifa wa UVCCM, Kheri Denise James
mara baada ya kumaliza kutembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya cha
Kazogolo katika halmashauri ya mji wa Nzege .
Kheri
alisema kitendo cha serikali ya awamu ya tano kupeleka jumla ya
shilingi milioni mia tano toka serikali kuu oktoba mwaka huu kwa ajali
ya ujenzi wa kituo hicho ni kielelezo kuwa serikali inajali maisha ya
wetu wake .
"UVCCM
tumeridhishwa na ujenzi wa miradi ya afya katika halmashauri za mji wa
Nzega na halmashauri ya nzega vijijini.Ilani ya uchaguzi ya chama
imetekelezwa kwa vitendo. Hii ndiyo tafsiri halisi ya hapa kazi "Alisems
Kheir .
Aidha alisema
kazi ya kuwatumikia wananchi haina mjadala badala yake inamhitaji kila
kiongozi dhamana kuwa nafasi yake kuwajibika na kuwatumikia wananchi.
"Kuimarika
kwa huduma za jamii na watu kupata huduma bora ndiyo malengo ya kisera
yanayotakiwa kufanikishwa. Tuna wajibu kila mmoja kwa nafasi yake
kumsaidia Rais na serikali yale "Alisisitiza
Kheri akiwa mkoani Tabora ametembelea mradi mkubwa wa usambazaji maji tokaziwa
Victoria mkoani mwanza kupitia shinyanga hadi Tabora,kuona
maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya kazogolo na kuzumgumza na wananchi
katika halmashsuri ya mji wa nzega na nzega vijiijini.
No comments:
Post a Comment