Na Mauwa Muhammed, Zanzibar
Taasisi
zisizo za kiserikali zimezindua mradi wa uwajibikaji katika jukumu la utoaji
wa huduma za jamii kwa umma
zinazotekeleza mamlaka ya maendeleo ya serikali za mitaa.
Akizindua
mradi huo wa kuinua uwajibikaji katika utoaji wa huduma Mkurugenzi Mtendaji wa
TAMWA, Mzuri Issa, huko katika ofisi yao iliyopo Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.
Amesema
mradi huo unahitaji mashirikiano ya pamoja na mamlaka ya Halmashauri na ofisi
za Wilaya ambazo ndizo zinazosimamia utoaji wa huduma kwa jamii kupitia
utaratibu mpya wa ugatuzi wa madaraka.
Amesema
miongozi mwa mambo yanayohimizwa katika kutekeleza mradi huo ni kuimarisha
mifumo ya kitasisi na sheria ili kuirahisishia ushirikishwaji imara kwa
wananchi kuanzia upangaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo katika maeneo
yao.
Mradi
huo unashirikisha wilaya sita za Zanzibar, unatekelezwa
na TAMWA kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wandishi wa habari za
maendeleo Zanzibar (Wahamaza) na jumuiya ya uhifadhi wa mazingira pemba
(Ngeraneko).
Wilaya
wenyewe ni Kaskazini A,Kati,Kusini kwa Kisiwa cha Unguja Ungja na
Wete,Chake Chake na Micheweni kwa Wilaya za Pemba ambapo
mradi huo utachukua miezi kuminatano.
Bi
Asha Aboud Muwasilishaji wa ripoti ya utafiti waliofanya wa uwiyano wa sheria
ya serikali za mitaa Zanzibar na sera za utawala bora kumebainika kuwepo na
kasoro katika suala la ushirikishwaji wananchi katika mipango inayohusu
maendeleo yao.
Alisema
moja ya msingi wa utawala bora ni ushirikishwaji wa wananchi wawe pamoja katika
kutoa mamuzi na pia wawe pamoja katika mapato na matumizi.
Ni
vyema kuona wananchi wana sehemu katika halamshauri wanatakiwa kushiriki na
kutelekezamikataba ya kimataifa kuwepo (Gender Equality).
Kuangalia
uwajibikaji wa viongozi na ufikiaji wa rasilimali na kuangalia miradi ya
maendeleo katika jamii
Amesma
lengo la ripoti hiyo ni kuangalia upatikanaji na ufikiaji wa huduma za kijamii
kama kuwepo shule na hospitali ambazo zinaruhusu makundi yote ya kijamii
yanafaidika hasa walemavu kuwepo miundombinu ya walemavu.
Pia
ripoti hiyo imeangalia ushiriki wa wanachi wakiwemo makundi malum katika
mipango ya maendeleo pia ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wa mipango ya
bajet.
Pia ripoti hiyo imeangalia huduma muhimu kwa
wananchi zinapatuikanaje na pia wananchi wanaridhika nazo na ikiwa hawaridhiki
nazo malalamiko yao wanayafikisha wapi.
Ametoa wito kwa malaka zinazohusia kutekeleza
sheria mpya ya upelekaji madaraaka ya kutoa majukumu ya utoaji huduma kutoka
serikali kuu kupeleka mikoani.
Amesema
ni vyema kutambua umuhimu wa kushirikishwa katikamasuala ya upangaji wa
bajet na utekelezaji wake.
Akichangia
katika mjadala wa ripoti hiyo mjumbe kutoka Wilaya ya Kusini Halida Nassor
alisema Halmashuri hazina uwazi kuhusu
mfuko wa Jimbo kwani hawajui unatumika vipi.
Alisema
kumekosekana umoja ndani ya jamii na ndio mana taratibu haziendi sawa.
Nae
mshiriki Ali Hamadi Afisa kutoka wilaya ya kati Unguja alisema wananchi
wanakosa muda wa kushirikishwa kutokana na kuwepo njia isiyo sahihi ya
kuwafikia ambapo hupelekea kuwepo
ushirikishwaji mdogo kwa jamii.
Alisema
ni vyema kutumia njia iliyo muafaka
ili kuwafikia wananchi wa makundi
yote bila kujali jinsia.
Nae
kwa upande wake Zawadi Pandu Vuai Diwani wa wadi ya makunduchi amesema sehemu
nyingi wananchi wamekuwa haawashirikihwi katika mipango ya maendeleo yao .
Alisema
ni vyema kuwepo mipango ili wanawake
waweze kuingia katika nafasi za kamati
katika Majimbo
Kwa
upande wake mshiriki Wahida Kondo
alisema katika Idara ya Utawala Bora
kumekuwepo Program tofauti kupitia vyombo vya habari za kuwaelimisha wananchi .
Alisema
kuna badhi ya maeno wanawake wamekuwa wanashindwa kujitokezakutokana na kukoza
elimu ya kujua umuhimu wa wajibu wao na wengine kukumbwa na majukumu ya
kifamilia.
Hivyo aliwataka wanawake kubadilika ili kuwendana na wakati wa sasa
ili kuzitambua haki zao.
No comments:
Post a Comment