April 23, 2018

WAANDISHI WA HABARI WASHAURIWA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUPAZA SAUTI ZA WANANCHI

AFISA Miradi wa TAMWA Zanzibar Bi. Asha Abdi, akifungua mafunzo ya Waandishi wa Habari Zanzibar kuhusiana na kutumia Vyombo vya habari pamoja na Mitandao ya Kijamii kupaza sauti za Wananchi kuchochea Uwajibikaji wa Watendaji, yaliowashirikisha waandishi wa habari za maendeleo Zanzibar na watumiaji wa mitandao ya kijamii Zanzibar, mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Watu wenye Ulemavu Welesi Zanzibar.

BAADHI ya Waandishi wa wakifuatilia Warsha ya Siku moja ya Mafunzo ya kuwawezesha Waandishi wa habari kutumia vyombo vya habari pamoja na mitandao ya Kijamii kupaza sauti za Wananchi na kuchochea uwajibikaji wa Watendaji, yaliofanyika katika ukumbi wa Watu wenye Ulemavu welesi, yalioandaliwa na Tamwa kwa kushirikiana na Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar.


Na Talib Ussi, Zanzibar

Waandishi wa habari wameshauriwa kutumia mitandao ya kijamii katika kuandika habari zao ili kuongeza nguvu za kupaza sauti za wananchi juu ya matatizo yanayowakabili kwa lengo la kupatiwa ufumbuzi wa haraka.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisa kutoka chama cha Waandishi na Habari Wanawake Tanzania (Tamwa-Zanzibar), Asha Abdi Makame katika Mafunzo ya siku moja jinsi ya waandishi kuona umuhimu wa kutumia mitandao ya kijamii katika kuandika habari zao.

Alieleza kuwa wananchi wanamatatizo mengi yanayowakabili na endapo waandishi wa habari watatumia vyema mitandao ya kijamii ikiwemo twitter facebook,whatssap kwa kuunganyisha na vyombo vyao vya habari ikiwemo redio,tv na magazeti matatizo yaliomo katika jamii yanaweza kupatiwa ufumbuzi wa haraka kwani kutakuwa na nguvu pamoja na kasi ya vyombo hivyo kwa kutoa msukumo kwa viongozi kuwajibika.

“Leo mtu wa chini hajui anahaki gani katika serikali za mitaa lakini mkitumia mitandao ya kijamii na mkawafahamisha juu ya hilo basi wataelewa na kudai haki zao” alieleza Asha.

Alieleza kuwa ili dhana ya uwajibikaji iweze kufikiwa na kuleta tija katika jamii ni vyemaa wananchi kushirikishwa shughuli mbali mbali ziwe za jamii na katika ngazi maamuzi.

“Unapowasemea wanyonge mtakuwa mmetimiza ile dhana ya tasnia yenu ya kuwasemea wasiokuwa na sauti” alieleza Asha.

Akifunga Mafunzo hayo Naibu Mkurugenzi wa habari Maelezo Juma Muhamed Salum ameitaka Jumuiya ya waandishi wa habari za maendeleo Zanzibar wahamaza kuwapatia mafunzo Viongozi wa Serikali na wajumbe wa baraza la wakilishi juu ya umuhimu wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutangaza kazi zao.

“Ni vyema Wahamaza baada ya kuwapatia mafunzo haya waandishi , mjipange kuwapatia mafunzo Viongozi wetu kwani jamii wanahitaji kujuaa nini wanafanya” alieleza Naibu huyo.

Alisema kuwa Mitandao ya kijamii mbali na kurahisisha habari kufika kwa urahisi na haraka lakini wako baadhi wengine hutumia mitandao kinyume na malengo yake ambapo hupelekea uvunjifu wa amani.

Mapema katibu mkuu wa Jumuiya ya waandishi wa Habari za maendeleo Zanzibar (Wahamaza) Salma Said aliwaambia waandishi wa habari muda umefika kuunganisha taarifa zao kwenye mitandao ya kijamii ili kuwa na wasomaji wengi zaidi.

Mafunzo hayo yamendaliwa na Jumuiya ya waandishi wa habari za Manendeleo Zanzibar (Wahamaza) ambayo ni mshiriki mmojawapo wa watekelezaji wa mradi wa kuinua uwajibikaji katika mpango wa ugatuaji wa madaraka Zanzibar. Washiriki wengine katika mradi huo unaofadhiliwa na ZANSAZP, ni Tamwa na Jumuia ya Kuhifadhi maliasili za asili Pemba (NGERANECO).

No comments:

Post a Comment

Pages