May 12, 2018

IDADI YA MABAHARIA WA ZANZIBAR YAPUNGUA

Mmiliki wa Kampuni ya Danaos, Ali Mzee Yusouf, akiwa katika picha ya pamoja na mabaharia wa Tanzania huku wakiwa wameshika fulana maalumu ambayo waliweka saini ya kupiga vita dawa za kulevya kwa kupitia kampuni yao. Hafla hiyo ilifanyika Chukwani Zanzibar. (Picha na Talib Ussi).

Na Talib Ussi, Zanzibar
Mmiliki wa  Kampuni ya  Danaos ambayo inamiliki chuo cha mabahari Zanzibar  Ali Mzee Yusouf amesema kuwa idadi ya mabahari wanaofanyakazi katika meli duniani kutoka Zanzibar imeshuka kutoka 1000 hadi 200 kutokana na baadhi kukamatwa na usafirishaji wa dawa za kulevya.
Yusouf aliyazungumza hayo huko katika chuo cha Mabaharia Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar wakati wakizindua tamko maalumu la kupinga usafirishaji wa madawa ya kulevya kupitia mabaharia wa Tanzania na Zanzibar kwa ujumla wake.
“Usafirishaji wa dawa za kulevya umetushushia hadhi yetu kwani kampuni yetu ilikuwa inaminiwa duniani kote lakini sasa tunaona athari yake” alieleza Mzee Yusouf.
Alieleza kuwa zaidi ya mabahari saba (7) wamekamatwa wakiwa na madawa ya kulevya wakiwa safarini mara nyingi kutoka Brazil kuelekea bara la Ulaya.
Akizungumza katika shughuli hiyo Mwanasheria ya kampuni hiyo Abdallah Juma Muhammed alisema kutokana na wingi wa usafirishaji wa madawa hayo, imeundwa sheria kama Mtanzania mmoja akikutwa na madawa na Watanzania wote wanashushwa katika meli.
Kutokana na hali hiyo aliwaomba mabaharia walikuwepo hapo katika tukio hilo kujitambua wanalokwendea na kuwajingiza katika majanga ambayo hupoteza taaswira ya maisha yao.
“Tunajua soote tunapokwenda ubaharia familia zetu zoote zinategemea manufaa lakini jee tukikamatwa na madawa nikwamba mfumo mzima wa maisha ya familia tumeua baada ya kututegemea sasa tutawatia matatizo” alieleza Mwanasheria huyo.
Alisema kila kepteni wa meli ya nje sasa hivi anakataa kupokea mabaharia kutoka Tanzania kutokana na uharamia huu ambao umeingia wa kusafirisha madawa ya kulevya.
Sambamba na hilo aliwataka mabaharia woote kutoka Tanzania kuwa askari kwa ajili ya kulijengee taifa taaswiraa bora ili matukio hayo kwa watanzania yasitokee tenna.
Kwa upande wake Kepten Stelios Petronions ambaye ni mwalimu wa chuo cha mabaharia Zanzibar (ZDMMI) alieleza kuwa mtandao wa kusafirisha madawa ya kulevyo ni mkubwa na unambinu nyingi na kuwataka mabaharia wa Tanzania wasiwe rahisi kuhadalika usafirishaji wa madawa ya kulevya.
“Hawa mabwana ambao wanafanyabiashara hii wananguvu na wanakila uwezo kwa hiyo tnakazi ngumu ya kupambana nao lakini tukishirikiana makepteni na Mabaharia kwa ujumala tunaweza kuhimili kama sikushinda kabisa” alieleza Kepteni huyo.
Aliwaambia mabaharia kabla ya kujibu chochote mtu anapopokea ujumbe kutoka kwa waharamia hao ni vyema akafuata taratibu usalama ili asijeakajiingiza katika majanga.
Naye Mwakili wa Mamlaka ya Usafirini Baharini Zanzibar khamis Mhummed Ali aliwaomba mabaharia hao kuacha kazi hiyo kwa kufanyakazi hiyo ni kupoteza taaswira ya Taifa.
“Tusiwe na utajiri wa haraka kwani tunaweza hata tukapoteza maisha yetu” alieleza Ali.
Alieleza kuwa ni vijana wangapi leo wanapoteza ajira hiyo kutokana wenzao kukutwa na madawa na kushushwa na huku wengine wakisalia jela katika nchi mbali mbali duniani ikiwemo Brazili, Itali na Morishiaz.
“Hawa wauzaji ni wajanja sana, wanaweza kukupa mzigo mara moja hadi mbili lakini mara ya tatu wao wanakukamatisha kwani lengo lao ni kukuharibia” alileza Ali ambaye ni Mkaguzi wa Meli.

No comments:

Post a Comment

Pages