May 29, 2018

RAIS DKT. MAGUFULI AWAANDALIA FUTARI WAGENI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi walioshiriki katika futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa amekaa  na Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa wa pili kutoka kulia, Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilal pamoja na viongozi mbalimbali walioshiriki Futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubery mara baada ya kufuturu Ikulu jijini Dar es Salaam. wa pili kutoka kulia ni Waziri wa Dini kutoka Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek
Wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wastaafu pia walishiriki katika futari hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kufuru Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa mara baada ya kufuturu Ikulu jijini Dar es Salam. PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

Pages