June 01, 2018

BENKI YA CRDB YAKABIDHI ZAWADI WASHINDI WA KAMPENI YA SHUHUDIA KOMBE LA DUNIA NA TEMBO CARD VISA

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza katika hafla ya kutoa zawadi kwa washindi wa Kampeni ya Shuhudia Kombe la Dunia na Tembo Card Visa.











Mshindi wa kampeni ya ‘Shuhudia kombe la Dunia na Tembokadi viza’ inayoendeshwa na Benki ya CRDB Tanzania, Emmanuel Mseja (katikati), ambaye ni kipa wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba SC, akipokea zawadi ya runinga na kisimbusi cha DStv wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam Juni 1, 2018.





NA MWANDISHI WETU
MLINDA mlango wa Klabu ya Soka ya Simba, Emmanuel Mseja ameshinda runinga na king’amuzi cha DSTV kwenye kampeni ya ‘Shuhudia kombe la Dunia na Tembokadi viza’ inayoendeshwa na Benki ya CRDB Tanzania.
Ushindi wa Mseja ulitangazwa Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei alipowakabidhi zawadi washindi wa wiki tatu za mwanzo za kampeni hiyo.
Akizungumza kabla ya kugawa zawadi hizo, Dk. Kimei alisema kwa wiki tatu walipatikana washindi 15 kati yao watatu walishika namba moja kila wiki watakabidhiwa tiketi kwa ajili ya safari ya Russia kushuhudia kombe la dunia.
“Kila wiki tulipata washindi watano, waliochanja sana walishika nafasi ya kwanza na hao watakwenda kushuhudia mechi za ufunguzi za kombe la dunia huko Russia.
“…Safari ya Russia imelipiwa kila kitu mshindi anatakiwa kwenda kufurahia maisha akiwa huko,” alisema Dk. Kimei.
Washindi watatu watakaokwenda Russia kuangalia mechi za kombe la dunia ni Mohamed Kinjenge, Hemant Josh na Nuru Kisome.
Akizungumzia ushindi huo Mseja alisema anafurahia huduma za benki hiyo na kwamba hakutegemea kuwa mshindi licha ya kwamba ni utaratibu wake wa kawaida kuchanja.
“Mimi huwa nachanja ninapofanya manunuzi mara nyingi sana sikuwa najua kama siku moja nitashinda namshukuru Mungu na kuwapongeza wlaiobuni shindano hili. Nitaendelea kuchanja naamini naweza kuipata safari ya Russia,” alisema mlinda mlango huyo wa mabingwa wa soka Tanzania.
Washindi wengine waliopata seti ya luninga na kingamuzi cha DSTV ni Zubeda Chande, Mgullu Mgullu, Mats Idvall, Jenny Correia, Mueen Ibaya, Hassan Mwinyigogo, Elias Patrik, Anthhony Shayo, John Mwangulangu, Karen Kanza na Wetermack Batanyita.
Kwa mujibu wa Dk. Kimei lengo la kampeni hiyo ni kuwajengea wateja wao utamaduni wa kutumia kazi zao kufanya malipo na manunuzi mtandaoni.

Kampeni ya shuhudia kombe la dunia na Fifa mwaka 2018 na Tembokadi Visa ilizinduliwa mwanzoni mwa Aprili kwa benki ya CRDB kushirikiana na Visa International miongoni mwa wadhamini wa kombe la dunia.

No comments:

Post a Comment

Pages