June 07, 2018

BENKI YA CRDB KUIMARISHA USHIRIKIANO NA JESHI LA POLISI NCHINI

 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro, akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam Julai 7, 2018.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro, akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia), wakati uongozi wa benki hiyo ulipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB pamoja na Maofisa wa Jeshi la Polisi wakiwa katika mkutano.
 Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB wakifuatilia majadiliano kati ya IGP, Sirro na Dk. Kimei.
 Baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Polisi wakiwa katika mkutano wa IGP na Uongozi wa Benki ya CRDB.
Maofisa wa Benki ya CRDB.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro, akizungumza na uongozi wa Benki ya CRDB ulipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na maofisa wa Jeshi la Polisi alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo. Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Bi. Esther Kitoka.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro, akionyesha Kadi ya TemboCard Visa Infinite, aliyokabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia), wakati uongozi wa Benki ya CRDB ulipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Viva Tower, Naomi Mwamfupe.
Picha ya pamoja.

Na mwandishi Wetu

Uongozi wa Benki ya CRDB ukiongozwa na Dkt.Charles Kimei umetembelea makao makuu ya Jeshi la Police Jiji Dar es Salaam.

Katika mazungumzo kati ya pande mbili Dkt. Kimei aliahidi kudumisha ushirikiano uliopo kati ya benki ya CRDB na  Jeshi la Polisi, Pia Dokta kimei alitoa wito kwa askari wa jeshi hilo kuendelea kutumia huduma za Benki ya CRDB ikiwa ni pamoja na kujipatia mikopo ambayo riba yake imepungua hadi kufika 16%.

 Aidha kwa upande wake IGP Sirro ameipongeza Benki ya CRDB kwa huduma zake bora ambazo zimekuwa na tija kwa askari wa Jesh la Police.

IGP amesema kwa kupata kadi ya TcVisa Infinite atakuwa balozi  wa Benki ya CRDB. 

No comments:

Post a Comment

Pages