HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 18, 2018

MSOMI AONYA UBORA WA DAWA

Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Lucy Massoi, akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam wanaohusika na usafirishaji wa madawa na vifaa tiba ili viweze kufika kwa wakati katika hospitali kwa ajili ya kuboresha huduma za afya, mafunzo hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na chuo hicho kwa kushirikiana na taasisi ya Kuehne Foundation.

Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Lucy Massoi, akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.

Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Lucy Masoi (kushoto), akiwa na Meneja wa Progromu wa Taasisi ya Kuehne Foundation, Wolf Christian Noske.

Mratibu wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam wanaohusika na usafirishaji wa madawa na vifaa tiba ili viweze kufika kwa wakati katika hospitali kwa ajili ya kuboresha huduma za afya, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Omary Swallehe, akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo.

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Omary Swallehe, ambaye ni Mratibu wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam wanaohusika na usafirishaji wa madawa na vifaa tiba akichangia mada.

Washiriki wa mafunzo hayo.

Mshiriki wa mafunzo hayo akichangia mada katika warsha hiyo.

Mwezeshaji kutoka JIS International, Harrison Mariki, akitoa mafunzo katika warsha hiyo.

Mwezeshaji kutoka JIS International, Harrison Mariki, akitoa mada katika warsha hiyo.

Picha ya pamoja. 


NA MWANDISHI WETU

NCHI ya Tanzania inapoteza dawa nyingi za binaadamu na baadhi zinawafikia walengwa nje ya wakati zikiwa na ubora hafifu. 


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya siku tatu kuhusu afya ya binaadamu na miundombinu yake, Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Lucy Massoi alisema usafirishaji wa bidhaa hizo unakwamishwa na miundombinu ya nchi yetu.

Alisema ufinyu wa miundombinu unasababisha watanzania wengi wa vijijini kutumia dawa zenye ubora hafifu na zinazokaribia kuisha muda wake huku dawa nyingi zikimaliza muda wa matumizi kabla ya kutumika.

"Uduni wa kusambaza dawa unatokana na uhaba wa usambazaji wa dawa hizo... Naamini semina hii washiriki wake watakuja na ujumbe utakaosaidia kuondoa tatizo hili na watanzania wote watapata dawa bora Kwa wakati.

"Sisi Chuo Kikuu Mzumbe jukumu letu ni kufundisha, kufanya tafiti, kushauri kitaalam na kutangaza matokeo ya tafiti za kisomi, hivyo tunalo jukumu la kutafuta ufumbuzi wa matatizo na changamoto za jamii kitaifa na kimataifa.

"Ni kweli kwamba suala la afya ya jamii na miundombinu yake ni eneo muhimu kwenye maisha yetu ya kila siku, nawatakia majadiliano mema yatakayokuja na matokeo chanya," alisema Dk. Massoi.

Mratibu wa semina hiyo, Dk. Omary Swallehe alisema Wataalam wa Chuo Kikuu Mzumbe wakishirikiana na Taasisi ya Kuehne wameona changamoto inayoikabili sekta ya afya ya binaadamu hasa suala la ufikishaji wa dawa na miundombinu yake.

Dk. Swallehe alisema semina hiyo inawashirikisha watumishi wa serikali na Sekta binafsi watakaokuja na njia sahihi ya nini kifanyike ili watanzania wa vijijini wapate dawa bora Kwa wakati sahihi.

No comments:

Post a Comment

Pages