WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania itaendeleza
ushirikiano na Serikali ya Kuwait katika sekta mbalimbali ikiwemo ya
usafiri wa anga.
Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Agosti 3, 2018) wakati alipokutana na Balozi wa Kuwait nchini, Balozi Jasem Al Najemkatikamakazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Balozi
Al Najem ambaye anamaliza muda wake, amekutana na Waziri Mkuu kwa lengo
la kumuaga na kwamba leo anatarajia kuondoka nchini na kurejea Kuwait.
Waziri
Mkuu amemshukuru balozi huyo kwa ushirikiano alioutoa Tanzania katika
kipindi chote cha uwakilishi wake na kwamba nchi hizo zinatarajia kuanza
ushirikiano katika usafiri wa anga.
Amesema
Kuwait ni moja kati ya nchi rafiki, ambayo imeshirikiana na Tanzania
katika uboreshaji wa shughuli za maendeleo kupitia Balozi Najem, hivyo
wataendelea kumkumbuka.
“Balozi
Najem amejitoa sana katika kuwasaidia Watanzania hususan kwenye miradi
ya huduma za jamii kwa kupeleka maji mashuleni, vituo vya afya, zahanati
na hospitalini,”.
“Pia
Ubalozi wa Kuwait umesaidia kuleta vifaa tiba katika Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete na madaktari katika baadhi ya hospitali nchini.
Ushirikiano huu umeleta tija sana,” amesema.
Waziri
Mkuu amesema mbali na miradi hiyo ya huduma za jamii, pia balozi huyo
ameshiriki kuendeleza Sekta ya utalii nchini kwa kuleta watalii wengi
kutoka nchini Kuwait kuja Tanzania.
Waziri
Mkuu meongeza kuwa Balozi Al Najem ameshiriki kikamilifu katika
kuratibu shugughuli zote za maendeleo kati ya nchi hizo mbili ikiwa ni
pamoja na kuunganisha sekta binafsi.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amemuhakikisha balozi huyo kwamba Tanzania itaendelea
kuimarisha ushirikiano wake na Kuwait na kwamba ipo tayari kumpokea
mwakilishi mwingine.
Kwa upande wake,
Balozi Al Najem ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa
ushirikiano iliyompa katika kipindi chote alichokuwa akiiwakisha
Serikali ya Kuwait nchini.
Amesema
tangu alipowasili nchini amekuwa akipewa ushirikiano mkubwa na viongozi
wote wa Serikali jambo lililomrahisishia utekelezaji wa majukumu yake
nchini.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, AGOSTI 3, 2018.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na mazungumzo na Balazi wa Kuweit Mh Jasem
Ibrahim AI Najem ,ambaye amemaliza muda wake .Balozi Jasem. amekutana
na Waziri Mkuu kwa lengo la kumuaga leo Julai 3/2018 Jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na Balozi wa Kuweit Nchini Tanzania
.Jasem Ibrahim AI Najem, ambaye amemaliza muda wake .Balozi Jasem.
amekutana na Waziri Mkuu kwa lengo la kumuaga leo Julai 3/2018 Jijini
Dar es Salaam.


No comments:
Post a Comment